Tuesday , 27 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kigogo ofisi ya RC Mwanza mikononi mwa Takukuru
Habari za SiasaTangulizi

Kigogo ofisi ya RC Mwanza mikononi mwa Takukuru

Spread the love

KIGOGO katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mfanyabiashara wa vifaa vya maabara jijini hapa. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Watumishi katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikiwa na wafanyabiashara kwamba wanaombwa fedha za rushwa, ambapo taarifa zinaeleza kuwa mmoja wa kigogo kwenye ofisi hiyo amekuwa akiwakingia kifua.

Kigogo aliyekamatwa na Takukuru, ni mchumi mwandamizi katika ofisi hiyo, Kaswalala Elisha ambaye alitiwa mbaroni Novemba 16 mwaka huu baada ya kupokea kiasi cha Sh. 300, 000 kutoka kwa mfanyabiashara mmoja ambaye hajatajwa jina lake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini humo, Naibu Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mwanza, Emmanuel Stenga alisema mtuhumiwa huyo amefanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya 2007.

Alisema mtuhumiwa huyo kwa kushirikiana na mtu mwingine ambaye bado anatafutwa kwa pamoja waliomba pesa hiyo kutoka kwa mfanyabiashara huyo wa vifaa vya maabara jijini hapa.

“Mtu mwingine ambaye walikuwa nae alijifanya usalama afisa usalama wa Taifa na kumtishia mfanyabiashara huyo wa vifaa vya maabara shule za sekondari kwamba anafanyabishara kwa njia za magendo.

“Watu hao walimueleza mfanyabiashara huyo kwamba, wana majalada yake ya uchunguzi kwa vile anafanya biashara bila kulipa kodi, anauzia serikali bidhaa feki ambazo anaziingiza kwa njia za panya hivyo ili wamlinde asichukuliwe hatua awape milioni tano ( 5, 000, 000),” amesema Stenga.

Naibu huyo wa Takukuru aliendelea kueleza kuwa baada ya kiasi hicho kutajwa waliendelea kupunguziana mpaka kufikia kiasi cha Sh. 300, 000.

Stenga alisema katika harakati za kuhakikisha wanaipata fedha hiyo kwa muda wa siku mbili kati ya Novemba 15 na 16, Kaswalala na mwenzake walikuwa wakiendelea kufuatilia kwa kupiga simu mara kwa mara kwa mfanyabiashara huyo.

“Mtuhumiwa huyu kuonyesha amebobea alimuita (mfanyabiashara) ofisini kwake (ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza) na kumsomea tuhumu zake na wakati wanaendelea na mazungumza ndipo mtuhumiwa mwingine anaesakwa alipoingia ambapo Kaswalala alimwamba ni mwenzake waliekuwa wakishirikiana kumchunguza,” alisema Stenga.

Stenga alisema kuwa, Novemba 16 mwaka huu, mchumi huyo mwandamizi alipokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mfanyabiashara huyo ndipo aliingia mikononi mwa maafisa wa Takukuru.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo imekuwa ni kawaidia yake kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wananchi na wafanyabiashara wakubwa na wa kati.

Hata hivyo, uchunguzi wa tuhuma hizo bado unaendelea, ambapo mchumi huyo mwandamizi ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kujibu tuhuma zinazomkabili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!