Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Ummy aionya bodi mpya ya TMDA
Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy aionya bodi mpya ya TMDA

Spread the love

BODI mpya ya ushauri ya Wizara ya Afya kwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imetakiwa kuisimamia mamlaka hiyo na kuacha kufanya kazi ya kipolisi kwa wenye viwanda vidogo na vya kati badala yake kuwawezesha kushamiri kwa biashara na uwekezaji nchini Tanzania. Anaandika Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Agizo hilo limetolewa na Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto jijini Dodoma leo Jumatano tarehe 17 Juni 2020 alipokuwa akizindua bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti Eric Shitindi.

“Nimekuwa nikieleza TMDA haipaswi kufanya kazi ya kipolisi hususani kwa wenye viwanda vidogo na vya kati, mnapochukua maamuzi haya mnatakiwa mjiulize je yanachangia kuwezesha uendelevu wa uwekezaji au biashara katika ukuaji wa uchumi wa viwanda?” amesema Waziri Ummy.

Amesema, jukumu kubwa la TMDA ni kulinda afya ya jamii kwa kudhibiti ubora, usalama na udhibiri wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi na kuwataka wasiongeze tozo kubwa ili kupata makusanyo makubwa.

Kuhusu tozo zilizofutwa, Waziri Ummy amesema, kupitia bodi iliyomaliza muda wake, walifanikiwa kufuta tozo zaidi ya 20 ambazo zilikua zinawaumiza wazalishaji na wafanyabiashara za dawa, vipodozi na vyakula lengo likiwa ni kumpunguzia gharama mtumiaji wa mwisho.

Ameyataja mafanikio mengine makubwa ya TMDA ni kutambulika na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa moja ya Taasisi bora ya udhibiti dawa ambapo imefikia hatua ya umahiri namba tatu pamoja na kuwa Mamlaka ya Udhibiti ya kwanza barani Afrika kufikia hatua ya tatu ya umahiri kwenye mifumo ya udhibiti wa dawa baada ya kuhakikiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO Maturity Level 3 Regulatory Authority).

Amesema, kuweka mifumo ya utendaji kazi ambayo imefikia kiwango cha ISO 9001:2015 toka mwaka 2009; Maabara yake kuweza kufikia viwango vya ISO/IEC 17025:2015 nakupa ta ithibati ya WHO (WHO Prequalified Laboratory); Kuanzisha Ofisi za Kanda kwenye mikoa 8 kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kujenga jengo la Ofisi na Maabara, Kanda ya Ziwa – Mwanza.

https://youtu.be/bbX3ZtoyecA

Hata hivyo, Waziri Ummy ameishukuru bodi iliyomaliza muda wake ambayo ilikua chini ya Mwenyekiti Balozi Ben Moses na wajumbe wake kwa kufanikisha mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha cha utendaji wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!