Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Kanyasu ataka Chuo cha Wanayamapori kutoa mafunzo bora  
Habari Mchanganyiko

Waziri Kanyasu ataka Chuo cha Wanayamapori kutoa mafunzo bora  

Spread the love

CONSTATINE Kanyasu, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ameitaka Bodi mpya ya magavana wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori (Mweka), kuhakikisha wanatoa mafunzo yenye ubora na kukidhi mahitaji kulingana na vipaumbele vya Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Moshi … (endelea).

Kauli hiyo imetelewa wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Magavana iliyofanyika katika chuo hicho, mkoani Kilimanjaro. Waziri Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangala ameteua wajumbe sita kwenye bodi hiyo walioteuliwa baada ya Rais John Magufuli kuongeza muda wa miaka mitatu kwa mwenyekiti wa bodi hiyo, Prof. Faustine Bee.

”Wote tunajua sekta ya utalii nchini imepata mtikisiko mkubwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona, kutokana na uzoefu tuliopata ni vyema bodi hii ikaelekeza chuo kuandaa mitaala mahususi itakayojielekeza zaidi kwenye matumizi ya teknolojia na usimamizi wa wanyamapori na utalii, ili majanga yanapojitokeza tuweze kukabiliana nayo,” amesema Kanyasu.

Costatine Kanyasu, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

Kanyasu amemwagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk. Aloyce Nzuki kukabidhi chuo hicho vitalu vilivyo wazi kwa ajili kukisaidia kutoa mafunzo kwa wataalam wa uwindaji wa utalii.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki aliitaka bodi ya chuo hicho, kutengeneza kwa haraka utaratibu wa kutoa wataalam wa uwindaji wa utalii.

Amesema, baadhi ya waliopo kwa sasa ni wachache katika fani hiyo na kwamba hawakidhi mahitaji yaliyokusudiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!