Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru aongeza kiwewe CCM
Habari za Siasa

Dk. Bashiru aongeza kiwewe CCM

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk. Bashiru Ally
Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimerudishwa nyuma tarehe ya kutaja majina ya waliopitishwa kugombea ubunge, udiwani na uwakilishi visiwani Zanzibar. Anaripoti Brightness Boaz, Dar es Salaam…(endelea).

Majina ya wateule wa chama hicho wataogombea kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020 yatatajwa Alhamis wiki hii (tarehe 20 Agosti 2020) badala ya tarehe 22 Agosti 2020.

Kwenye taarifa yake wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano kuhusu Uchaguzi Mkuu, jijini Dodoma Dk. Bashiru Ally ambaye ni Katibu Mkuu wa CCM amesema, Alhamis wiki hii ‘mambo hadharani.’

“Tarehe 20 Agosti 2020 tutafanya kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) na siku hiyo tutajua walioteuliwa,” amesema Dk. Bashiru.

Dk. Bashiru amewataka watia nia wote kutokuwa mbali na maeneo yao ya kugombea ili majina yao yatakapotoka wakachukue fomu ya kugombea katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ili wazijaze mapema kwa ajili ya kupisha zoezi la uteuzi wa wagombea litakalofanyika tarehe 25 Agosti 2020.

“Niwaombe watia nia wote wa viti maalum na majimbo kutokuwa mbali na maeneo yao, wabaki vituo vyao vya uchaguzi sababu tukitoa majina inabidi wachukue fomu na kuzijaza na ili tarehe 25 warudishe fomu kwa ajili ya uteuzi,” amesema Dk. Bashiru.

Leo Jumanne tarehe 18 Agosti 2020 Kamati Kuu ya NEC inapitia taarifa za wagombea zilizochambuliwa na Sekretarieti ya NEC, kikao hicho kitamalizika kesho tarehe 19 Agosti 2020.

Jana tarehe 17 Agosti 2020 Sekretarieti ya NEC ilichambua na kuandaa nyaraka za wagombea, ambapo taarifa hizo zinafanyiwa kazi na Kamati Kuu ya NEC inayoketi leo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!