Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge CUF wakwama kurudi bungeni
Habari za Siasa

Wabunge CUF wakwama kurudi bungeni

Stephen Kagaigai, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Spread the love

KATIBU wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Stephen Kagaigai amesema kuwa katika maamuzi ya mahakama hakuna sehemu imesema wabunge 8 wa CUF waliofutwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge wapewe Ubunge tena, anaandika Hamis Mguta.

Taarifa iliyotolea na Kagaigai kuwa amekuwa akiona kwenye mitandao ya kijamii na katika vyombo vya habari taarifa mbalimbali zikisema kuwa wabunge hao ambao walivuliwa uanachama na CUF kuwa wanatakiwa kurudishiwa ubunge wao na kudai hakuna jambo la namna hiyo kwa kuwa nafasi zao tayari zilijazwa na Tume ya Uchaguzi.

Amesema kuwa taarifa zinazosambaa kuwa wabunge hao wamerejeshwa bungeni kwa maamuzi ya mahakama ni za upotoshaji.

“Mnamo tarehe 10 Novemba 2017, Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam umetoa uamuzi wa awali katika shauri (Misc Civil Application No: 479 of 2017) iliyofunguliwa na wabunge nane wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania wa viti maalum kupitia CUF.

“Uamuzi huo wa mahakama ni wa awali na ulitolewa kwenye pinga mizi la awali na uliwalenga walalamikiwa ambao ni Baraza la wadhamanini CUF na uongozi wake ambao uliamuru kuwa walalamikiwa wasitishe utekelezaji wa kusitisha uanachama wao na kutojadili swala lolote kuhusu uanachama wao hadi mahakama itakapomaliza kusikiliza shauri la msingi.

“Ni vyema ifahamike kuwa hakuna sehemu yoyote katika uamuzi wa mahakama inayoelekeza kuwa wanachama hao wanatakiwa kurudishiwa ubunge wao,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Awali, waliokuwa wabunge hao waliiandikia barua bunge kuweza kufahamishwa utaratibu utakaotumika kuwarejesha bungeni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!