Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Vituo vya afya vya serikali vyapewa tahadhari
Habari Mchanganyiko

Vituo vya afya vya serikali vyapewa tahadhari

Kituo cha Afya Igoma, Mwanza
Spread the love

VIONGOZI wa vituo vya huduma za afya vya umma, wametakiwa kuchukua tahadhari ya matumizi ya fedha kulingana na bajeti ya serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Dk. Dorothy Gwajima,  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 21 wa kutathimini utekelezaji wa vipaumbele vya kisera katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dodoma leo tarehe 22 Disemba 2020.

Dk. Gwajima amesema, bado kuna malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu ukosefu wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini .

“Ili kufikia azma ya rais, sisi kama sekta ya afya inabidi kuongeza kasi katika uwajibikaji wa pamoja katika malengo tuliyoyaweka.

“Ni lazima tufanye upekuzi wa matumizi ya fedha za dawa, vifaa na maabara lazima ziheshimike na kufika kwa mgonjwa  ili wananchi watuamini na kuweza kutatua kero zao,” amesema.

Amesema, katika kutekeleza hilo, wizara  itatoa maelekezo ya kuongeza ufanisi katika uwajibikaji kuanzia kwa watumishi wote wa sekta ya afya, ngazi mbalimbali za usimamizi na uendeshaji.

Kuhusu tiba asili na tiba mbadala, Dk. Gwajima amesema zimekuwa zikisaidia katika kutibu magonjwa mbalimbali  kwa wananchi na hivyo serikali inakusudia kuimarisha  kitengo cha utafiti  wa tiba mbadala.

Dk. Festo Dugange, Naibu Waziri Ofisi ya Rais -TAMISEMI amesema, ili kufikia lengo la kuwawezesha  wananchi wote kuwa na bima ya afya, kunahitajika kuimarisha mifuko ya bima hiyo ili  kuwafikia wananchi wengi.

“Mfuko wa afya  ya jamii ulioboreshwa kwa sasa unachangia asilimia  tano ya wanufaika  wote waliojiunga  katika mifuko ya bima za afya nchini.

“Katika kipindi cha utekelezaji wa mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa  kuanzia Julai 2018, tumefanikiwa kusajili kaya 557,882 sawa na wanufaika 3,347,112 kufikia Novemba 2020,” amesema Dk. Dugange.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!