Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Virusi vya Corona vyauwa watu 1,000, Watanzania waishio China njiapanda
Habari Mchanganyiko

Virusi vya Corona vyauwa watu 1,000, Watanzania waishio China njiapanda

Watanzania waishio China wakiandamana kuomba kurudishwa nchini
Spread the love

WATANZANIA waishio nchini China,  wako njia panda baada ya kukwama kurejea nchini kufuatia mlipuko hatari wa Virusi vya Corona, vilivyopoteza maisha ya watu zaidi ya 1,000. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Baada ya mlipuko huo kuendelea kuwa tishio, Watanzania hao ambao kwa sasa wamefungiwa sehemu moja ili kunusuru usalama wa maisha yao, wameiomba Serikali ya Tanzania kufanya hima kuwarejesha nchini.

Akizungumzia kuhusu suala hilo, Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amesema Watanzania hao wako katika wakati mgumu kutokana kwamba, mamlaka nchini China zimeshauri wasisafiri kwenda eneo lolote, ili kukwepa kuambukizwa ugonjwa huo.

Balozi Kairuki amesema uamuzi juu ya maombi ya Watanzania hao kurejeshwa nchini haraka, unatakiwa kuangaliwa kwa umakini kutokana na hali halisi iliyokuwepo, ili kukwepa madhara zaidi.

“Uamuzi utakaofanywa lazima uangalie hali halisi, si busara kufanya maamuzi kwa mihemko. Na tujifunze kwa wenzetu hatua walizochukua na matokeo yake. Ili tusijekuwa na majuto makubwa zaidi,” ameshauri Balozi Kairuki.

Balozi Kairuki ameeleza kuwa, hata nchini Japani Watanzania wote walikuwa wazima, lakini walipoanza kuondolewa, wanafunzi watano walipata maambukizi ya ugonjwa huo, ambao pia waliwaambukiza wenzao watano.

Kutokana na changamoto hiyo, Balozi Kairuki amewataka ndugu, jamaa na marafiki wa wanafunzi hao kumuomba Mungu aendelee kuwalinda, huku akiwahimiza kuwapa moyo wahusika, ili wasikate tamaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!