October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kabendera aanza kuona nuru

Mwandishi Erick Kabendera akiwa mahakamani

Spread the love

MAZUNGUMZO ya kukiri makosa kati ya mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP) yapo kwenye hatua ya mwisho. Anaripoti Martin Kamote, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 11 Februari 2020, kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Faraja Nchimbi, Wakili wa Serikali Mkuu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega.

Wakili Nchimbi ameieleza mahakama hiyo, kuwa upande wa mashtaka na ule wa utetezi upo kwenye majadiliano ya kukiri kwa muda mrefu sasa na yanafikia mwishoni.

Wakili Nchimbi ameiomba Mahakama kufanya mazungumzo binafsi na mshtakiwa Kabendera ili mtuhumiwa akubali kukiri mashtaka yake na kuendelea na taratibu nyingine za kisheria.

Nchimbi ameiomba mahakama hiyo kuhairisha shauri hilo mpaka tarehe 17 Februari mwaka huu.

Wakili wa Utetezi, Jebra Kambole ameieleza mahakama hiyo kuwa upande huu haupingi jamhuri kuzungumza na mtuhumiwa huyu.

Hakimu Mtega ameruhusu mazungumzo hayo na kuahirisha shauri hilo mpaka tarehe 17 Februari 2020.

Mazungumzo hayo yapo kisheria kifungu cha 3 na kuongeza kifungu cha 194 A 194 H cha sheria ya Makosa ya jinani ya mwaka 1985 sura ya 20 (Plea Bargaining), ambapo mtuhumiwa anapewa nafasi ya kukiri na kuiomba msamaha na baadaye kuachiwa huru.

Hivyo huenda Kabendera huenda Jumatatu akaachiwa huru kutokana na mazungumzo hayo.

error: Content is protected !!