Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Urais Z’bar: Chadema kumsimamisha Said Mohamed
Habari za Siasa

Urais Z’bar: Chadema kumsimamisha Said Mohamed

Spread the love

BARAZA Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendelea (Chadema) kimependekeza kwa mkutano mkuu wa chama hicho, Said Issa Mohamed kuwa mgombea Urais wa Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea)

Mapendekezo hayo yamefanywa na baraza hilo leo Jumatatu tarehe 3 Agosti 2020 katika mkutano unaofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mkutano mkuu wa chama hicho utakaofanyika kesho Jumanne, utathibitisha jina hilo la Mohamed ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Zanzibar.

Akizungumza na wajumbe wa mkutano huo, Mohamed amesema, “mtaniunga mkono na kwa mara ya kwanza, kijana mdogo kabisa anakuwa Rais ndani ya nchi ya Zanzibar na dunia itashangaa.”

“Katika mapambano na ujasili mnanifahamu vya kutosha. Tunasema sasa basi. Tumeamua kuweka mgombea urais Zanzibar ni kutekeleza lengo la chama kuwa na mgombea urais wa Zanzibar na kwa mara ya kwanza, tunakwenda kushinda,” amesema Mohamed

Wajumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakisubiri kuanza kwa kikao hicho

“Naweza, nitumeni, niko tayari kupeperusha bendera ya Chadema upande wa Zanzibar. Wanasema mzigo mzito mpe Mnyamwezi lakini mzigo wa hatari ili ufike mpe Mpenda,” amesema

Baada ya kumaliza kujinadi, Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema aliwauliza wanaokubali pendekezo hilo walikubali huko watano wakipinga.

Mbowe amesema, Said Issa Mohamed amependekezwa kwenda mkutano mkuu.

Mohamed anakwenda kuchukuana na wagombea wengine akiwamo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi aliyepitishwa kuwania urais.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!