WANACHAMA 15 wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wamerudisha fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
CCM ilifungua zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu, sambamba na utafutaji wadhamini 250 kwa kila mtia nia wa kugombea nafasi hiyo, tarehe 15 Juni 2020. Zoezi hilo linatarajiwa kufungwa Jumanne ya tarehe 30 Juni 2020.
Hadi jana Ijumaa tarehe 26 Juni 2020, takribani makada 15 kati ya 30 waliojitokeza kugombea nafasi hiyo, walirejesha fomu za kugombea urais wa Zanzibar.
Wanachama hao wa CCM walizikabidhi fomu zao kwa Cassian Gallo’s , Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC, Idara ya Oganaizesheni Zanzibar, kwenye Ofisi Kuu ya chama hicho visiwani humo, iliyoko maeneo ya Kisiwandui.
Waliorudisha fomu ni, Balozi Ali Abeid Karume, mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume. Dk. Hussein Mwinyi, Waziri wa Ulinzi na Mtoto wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Dk. Ali Hassan Mwinyi.
Wengine ni, Shamsi Vuai Nahodha, aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Zanziba. Mhandisi Makame Mbarawa, Waziri wa Maji. Mbwana Bakari Juma, Mbwana Yahya Mwinyi, Omar Shehe Mussa, Mohamed Hijja Mohamed na Mohamed Jumanne.
Issa Suleiman Nassor, Abdulhalim Mohamed Ali, Khamis Mussa Omar, Rashid Ali Juma, Dk. Khalid Salum Mohamed, na Ayoub Mahmoud Mohamed.
Wanachama wengine 15 ambao hajarudisha fomu zao ni, Mussa Aboud Jumbe, Mtoto wa Rais Mstafu wa Zanzibar. Fatma Kombo Masoud, Hasna Atai Masoud, Iddi Hamad Iddi, Pereira Ame Silima, Shaame Simai Mcha, Hashim Salum Hashim na Ayoub Mohammed Mahmoud.
Wengine ni, Hussein Ibrahim Makungu, Bakari Rashid Bakari, Mohammed Aboud Mohammed, Mhandisi Hamad Yusuph Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani. Mmanga Mjengo Mjawiri, Khamis Mussa Omar na Rashid Ali Juma.
Wagombea wote 29 waliojitokeza ni;
- Mbwana Bakari Juma
- Balozi Ali Abeid Karume
- Mbwana Yahya Mwinyi :
- Omar Sheha Mussa
- Dk. Hussein Ali Mwinyi
- Shamsi Vuai Nahodha
- Mohammed Jaffar Jumanne
- Mohammed Hijja Mohammed
- Issa Suleiman Nassor
- Profesa Makame Mnyaa Mabarawa
- Mwatum Mussa Sultan
- Haji Rashid Pandu
- Abdulhalim Mohammed Ali
- Jecha Salum Jecha
- Dk. Khalid Salum Mohammed
- Rashid Ali Juma
- Khamis Mussa Omar
- Mmanga Mjengo Mjawiri
- Hamad Yussuf Masauni
- Mohammed Aboud Mohammed
- Bakari Rashid Bakari
- Hussein Ibrahim Makungu
- Ayoub Mohammed Mahmoud
- Hashim Salum Hashim
- Hasna Atai Masound
- Fatma Kombo Masound
- Iddi Hamadi Iddi
- Pereira Ame Silima
- Shaame Simai Mcha
- Mussa Aboud Jumbe
Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE & MwanaHALISI TV
Leave a comment