MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imeweka historia ya makusanyo ya mapato kwa Desemba 2020, kwa kukusanya Sh.2.088 trilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kiwango hicho cha makusanyo, hakijawahi kukusanywa katika historia ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Hayo yamesemwa leo Ijumaa tarehe 01 Januari 2021 na Kamishna Mkuu wa TRA, Dk. Charles Mhende wakati akitoa taarifa za makusanyo hayo.
Soma mchanganuo wote wa taarifa ya makusanyo ya Dk. Mhende;
Tusidanganyane. Sehemu kubwa ya kodi inayokusanywa ni kutoka taasisi za fedha. Benki zinakusanya kodi katika kila kitu. Kuanzia riba hadi fedha zinazochukuliwa hadi wateja kuuliza salio na kadhakika. ATM zinafanya kazi ya kukusanya kodi na wala si TRA
Simu za mkononi nazo kila kitu kodi – kutuma fedha hadi kuuliza salio hadi kutoa fedha na kadhalika. Ukusanyaji unafanywa na mawakala na wala si TRA ambao ni wapokeaji tu
Halafu kuna mamilioni ya waajiriwa katika makampuni na mashirika na serikali. Hawa wanakatwa PAYE kutoka mishahara yao na kuwasilishwa TRA
Kwa upande mwengine kiuna mamilioni ya wafanya biashara ambao wanakwepa matrilioni ya kodi wala hawaulizwi na TRA. Fika Kariakoo na kuona ni maduka mangapi wana mashine za risiti na kuzitumia? Haifiki hata asilimia moja. Tena hawalipi hata kodi ya mapato