Rais Magufuli awaapisha viongozi sita Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo Alhamisi tarehe 21 Mei 2020 amewaapisha viongozi sita aliowateua hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hafla ya kuwaapisha viongozi hao imefanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma asubuhi hii.

Viongozi walioapishwa ni; Dk. Godwin Mollel kuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wanawake Wazee na Watoto.

Dk. Mollel ameapishwa kuchukua nafasi ya Dk. Faustine Ndungulile ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Dk. Delphine Magere ameapishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani kuchukua nafasi ya Theresia Mbando ambaye amestaafu kwa mujibu wa utumishi wa umma.

Wengine ni; Dk. Jacob Kingu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Phaustine Kasike kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji na John Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya.

Pia, Rais Magufuli amemwapisha Brigedia Jenerali, John Mbungo kuwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru).

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo mawaziri na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE kwa habari zaidi 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo Alhamisi tarehe 21 Mei 2020 amewaapisha viongozi sita aliowateua hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma ... (endelea). Hafla ya kuwaapisha viongozi hao imefanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma asubuhi hii. Viongozi walioapishwa ni; Dk. Godwin Mollel kuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wanawake Wazee na Watoto. Dk. Mollel ameapishwa kuchukua nafasi ya Dk. Faustine Ndungulile ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Dk. Delphine Magere ameapishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani kuchukua nafasi ya Theresia Mbando ambaye amestaafu kwa mujibu wa utumishi wa umma. Wengine ni; Dk.…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram