JOHN Magufuli, Rais wa Tanzania, ameliagiza Jeshi la Polisi kumwachia huru msanii wa muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’ huku akimshauri kuporesha wimbo wake wa Wapo, anaandika Faki Sosi.
Ney wa Mitego alikamatwa na polisi mkoani Morogoro juzi usiku na kuleta jijini Dar es Salaam kwa madai ya kuimba wimbo uliokuwa na maneno yanayoikashifu serikali na viongozi wake.
Rais Magufuli kupitia kwa Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, Michezo, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Rais Magufuli amevutiwa na wimbo huo kutokana na kueleza hali halisi na kwamba ameshauri kuwa wimbo huo ungeendelezwa klwa kuwataja wakwepa kodi, wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya, na watu wanaofanya mambo yasiyofaa katika jamii.
Dk. Mwakyembe alidai kuwa Rais alimuambia kuwa: “Huyo kijana wako (Ney) aboreshe huo wimbo asiondoe chochote ila angoze aileze changamoto za jamii halafu aitike kama ulivyo wimbo wenye ‘wapo’… wauza madawa ya kulevya wapo… wakwepa kodi wapo…” alidai Dk Mwakyembe .
Dk Mwakyembe alikiri kuwa alishauriwa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kuhusu wimbo huo na kwamba aliwaambia wauwachie.
Baadhi ya mashairi yaliyokuwepo kwenye wimbo huo , “Hivi Uhuru wa Kuongea bado upo? Siamini nchi inaendeshwa kwa kiki! Nasikia kuna viongozi wamefoji vyeti? Wapooo! Mheshimiwa hivi unamjua Bashite kutoka Kolomije? We si Dokta wa kutumbua majipu?”
Leave a comment