Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba aelemewa Z’bar
Habari za Siasa

Prof. Lipumba aelemewa Z’bar

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF)
Spread the love

SIASA za upinzani Zanzibar, zinaelekea kumwelemea Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), na sasa anatupa lawama zake kwa Maalim Seif Sharif Hamad. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Maalim Seif ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, anatajwa na Prof. Lipumba kusababisha mkwamo wa demokrasia visiwani humo.

Prof. Lipumba akizungumza na wanahabari leo tarehe 21 Novemba 2019, Buguruni jijini Dar es Salaam, amesema Chama cha ACT-Wazalendo kimeenda kuwamaliza kabisa.

“Wamekuja kutumaliza kabisa baada ya jamaa (Maalim Seif) kuhamia ACT-Wazalendo, muasisi wake ni Zitto Kabwe ambaye anadai ni muumini wa ujamaa wa Mwalimu Nyerere.

“… na Maalim Seif anasema, kwamba Mwalimu Nyerere alifanya njama juu ya huu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar akilenga kuimeza na kuitawala Zanzibar, sasa hawa watu watakuwaje kwenye chama kimoja? na watawaambia nini Wazanzibar,” amesema.

Akizungumza kuhusu maazimio ya Baraza Kuu la Uongozi la CUF, Prof. Lipumba amesema, waliokuwa wanachama wa chama hicho waliohamia ACT-Wazalendo wakiongozwa na Maalim Seif, wamechangia kuyumbisha demokrasia visiwani humo.

“Uchaguzi wa 2015, CUF tulipata wawakilishi 27 Zanzibar na Baraza la Wawakilishi waliwappa vyeti kwa kuchaguliwa kuwa wawakilishi.

“Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi akafuta uchaguzi, tukakubaliana wawakilishi wote na madiwani wote wakafungue kesi, lakini tulipofika Zanzibar aliyekuwa Katibu Mkuu wetu (Maalim Seif Sharif Hamad) akazuia zisifunguliwe,” amesema.

Ameeleza, hata mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yasingeweza kufanyika kwasababu, wangekuwepo wawakilishi wao na wangezuia

Na kwamba, kuzuia kupeleka kesi mahakamani, ni sawa na kujipiga risasi mguuni na kuwa, kwenye vyombo vya kufanya maamuzi ya kisheria, CUF haipo.

Tarehe 18 Machi 2019, Maalim Seif aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, alihamia Chama cha ACT-Wazalendo muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuamua kuwa, Prof. Lipumba ni mwenyekiti halali wa chama hicho.

Mgogoro wa kiungozi ndani ya CUF, kati ya Prof. Lipumba na Maalim Seif, ulikomaa kutokana na Prof. Lipumba kutaka kurejea madarakani baada ya kaundika barua ya kujiuzulu uenyekiti wa chama hicho.

Miongoni mwa maazimio 16 ya baraza hili ni kuwa, wameitaka serikali kauacha tabia ya kuwakamata na kuwabambikizia kesi, baadhi ya waliokiwa wagombea wa chama hicho kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!