Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ndugai awaonya wabunge CCM, ataka Bunge ‘live’  
Habari za Siasa

Ndugai awaonya wabunge CCM, ataka Bunge ‘live’  

Bunge la Tanzania
Spread the love

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewataka wabunge wa chama tawala- Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokukaa kimya bungeni na watakaofanya hivyo “umeliwa na utakuwa umejimaliza.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia, amesema, Ofisi ya Bunge itahakikisha taarifa zinazohusu muhimili huo, zinawafikia kwa haraka wananchi kwani “tukijifungia ndani, tutakuwa hatusikiki kwa hiyo lazima Bunge hili lionekane.”

Ndugai amesema hayo leo Jumanne tarehe 10 Novemba 2020 bungeni jijini Dodoma, mara baada ya kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 la Tanzania.

Ndugai ambaye ni Mbunge wa Kongwa, amechaguliwa kwa kura 344 kati ya 345 na kura moja ikiharibika sawa na asilimia 99.7.

          Soma zaidi:-

Kikao hicho cha kwanza cha mkutano wa kwanza cha uchaguzi, kilisimamiwa na Mwenyekiti, William Lukuvi ambaye ni mbunge wa Ismani.

Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa, Spika Ndugai amemshukuru Mwenyekiti wa muda, Lukuvi “kwa kuifanya kwa weledi mkubwa kazi hii. Yeye ndiye mbunge amekuwepo mfululizo kuliko yoyote humu ndani.”

“Yeye (Lukuvi) hii ni mara ya sita. Uliyeingia mara ya kwanza, angalia njia kama inakufaa ili uwawakilishe wananchi wako. Na mtu aliyekaa mfululizo ni mimi mwenyewe,” amesema Spika Ndugai

Huku wabunge wakishangilia, Spika Ndugai akasema, “kukaa muda mrefu si jambo jepesi. Nawashukuru kwa kuaminiwa. Ni heshima kubwa sana kwa kuaminiwa.”

Job Ndugai, Spika wa Bunge la 12 la Tanzania

“Tunaowajibu mkubwa mbele yetu. Naamini kila mmoja anatambua wajibu wake, tutunge sheria zilizo bora, kuishauri serikali kwa ukweli na wazi,” amesem

Amesema, tarehe 5 Novemba 2020, wakati Rais John Pombe Magufuli akiapishwa kuwa Rais alisema uchaguzi umemalizika na “kwa hiyo, kuanza kuapishwa wabunge ni kuendelea kupigia msumari kwamba uchaguzi umekwisha, sasa ni hapa kazi tu na Mungu atubakiri.”

“Kazi yetu haitakuwa nyepesi, Bunge letu linapaswa kuwa la matokeo chanya kwa maendeleo ya Tanzania,” amesema.

Spika Ndugai amesema, mpango wa nchi, sheria, bajeti na mambo mengine yatapita bungeni, “chombo hiki ndicho mshauri wa serikali, Serikali itakuja kujibu hapa maswali. Uwajibikaji wa serikali ni hapa, naamini si kazi ngumu.”

Kuhusu wingi wa wabunge wa CCM ndani ya Bunge hilo, Spika Ndugai amesema, “ni kweli kabisa wabunge wengi wa Bunge la 12 wanatoka CCM, lakini hilo halimaanisha litakuwa la ndio, ndio, ndio au hapana hapana hapana.”

“Litakuwa Bunge la kutekeleza wajibu wake, miongoni mwao watateuliwa kuwa mawaziri na naibu mawaziri, niwahakikishie, hapa bungeni watawajibika kweli kweli, hakuna kubebana,” amesema

Akiendelea kutoa nasaha zake hasa kwa wabunge wapya, amesema “ukichagua kuwa mbunge bubu usiyesema, husemi, upo upo tu ili uonekane una nidhamu, umeliwa na utakuwa umejimaliza, wananchi wamekuchagua ili uwawakishe bungeni.”

Kuhusu taarifa kuwafikia wananchi, Spika Ndugai amesema “sisi tutajitahidi kuhakikisha taarifa wananchi zinawafikia haraka zaidi. Tukijifungia ndani, tutakuwa hatusikiki kwa hiyo lazima Bunge hili lionekane, lisikike mnavyoiambia serikali, msikike na serikali itasikika.”

Spika Ndugai amegusia wabunge wa upinzani akisema “ndugu zetu wa upinzani, mna haki zenu kabisa. Moja ya kazi ya kiti mnasikika na mliowengi mkiwaachia wachache wasikike shauri yenu.”

Akihitimisha salamu zake, Spika Ndugai akatoa tahadhali, “asije kukusogelea mtu umkopeshe, tulipata tabu sana katika Bunge lililopita, kwa hiyo mkikopeshana huko tusilaumiane.”

Kinachoendelea sasa bungeni ni Spika Ndugai kuwaapisha wabunge.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!