Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanaume waoga kupima ukimwi
Habari MchanganyikoTangulizi

Wanaume waoga kupima ukimwi

Spread the love

UTAFITI umebainisha kuwa wanaume wengi wamekuwa waoga kupima afya zao, hususani kupima Ukimwi jambo ambalo ni hatari zaidi kwa tofauti na wale ambao wanajitokeza kupima afya zao. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Ushauri huo umetolewa jana jijini Dodoma, na Mkurugenzi wa Uraghbishi na Habari TACAIDS, Jumanne Isango,  alipokuwa akifungua mkutano wa usambazaji wa matokeo ya Utafiti wa Kitaifa wa Viashiria na matokeo ya Ukimwi (THIS) wa mwaka 2016/17 na miongozo mingine ya kitaifa ya kuthibiti ukimwi kwa waandishi wa redio za kijamii nchini.

Isango alisema kuwa utafiti unaonesha kuwa  asilimia kubwa ya wanaume wamekuwa hawapimi afya zao hususani Ukimwi badala yake wamekuwa wakikwepa kupima na wengine kutumia afya za wake zao kama sehemu ya wao kuwa salama.

Akifungua mkutano huo Isango aliwataka waandishi wa redio za kijamii kuenddesha kampeini ya kuwashawishi na kuwelimisha wanaume faida ya kupima afya zao kwa hiari hususani kupima ugonjwa wa ukimwi pamoja na kuanza kutumia dawa za kufubaza virusi vya ukimwi.

Alisema kuwa mtu ambaye hajapima afya yake yupo katika hatari zaidi na hawezi kuwa na furaha ya maisha kama ilivyo kwa mtu ambaye tayari amepima afya yake na kujijua.

“Mtu ambaye amepima afya anayo furaha zaidi ya maisha kuliko mtu ambaye ajapima,pia mtu ambaye amegundulika anayo furaha kubwa ya maisha kwani tayari anajitambua na kujijua na kuanza kutumia dawa na yule ambaye anabainika kuwa hana virusi vya ukimwi anayo furaha zaidi kwani wanakuwa na uhakika wa kujua afya zao na kujikinga na maambukizi mapya,” alisema Isango.

Katika hatua nyingine Isango alisema kuwa katika kampeini ya kupima ukimwi kwa hiari TACAIDS inatarajia ifikapo 2020 kila asilimia 90 ya watanzania wawe wanatambua afya zao na wale ambao watakuwa wamebainika kuwa na virusi vya ukimwi watakuwa wanatumia dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi.

Akizungumzia kuhusu waandishi wa habari aliwataka waandishi wa habari kuwa makini katika utoaji wa taarifa hususani katika masuala mazima ya nayohusiana na ugonjwa huo wa ukimwi  hasa kwa upande wa takwimu.

Aidha alisema kuwa masuala ya ugonjwa wa ukimwi yaandikwe kwa kuzingatia mazingira husika ikiwa ni suala la kupanda kwa maambukizi au kushuka kwa maambukizi ili kuweka taarifa sawa ambazo haziwezi kuwachanganya wananchi.

Katika hatua nyingine  Isango aliwataka wamiliki wa vyombo vya habari pia kuwekeza nguvu zaidi kufungua redio za kijamii katika mikoa kwa lengo la kuongeza nguvu ya utoaji wa elimu kwa jamii katika Nyanja mbalimbali huku waandishi wa habari wakiwa msitari wa mbele katika utoaji wa elimu ya magonjwa mbalimbali pamoja  maendeleo kwa ujumla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!