Tuesday , 18 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi wamng’ang’ania Mtatiro, mwenyewe adai yupo Ngangari
Habari za SiasaTangulizi

Polisi wamng’ang’ania Mtatiro, mwenyewe adai yupo Ngangari

Spread the love

MWENYEKITI wa Muda wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatito ameendelea kubaki mikononi mwa Polisi huku akituhumiwa kwa kusambaza ujumbe unaomkashifu Rais. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mtatiro alitakiwa kuripoti Polisi jana asubuhi na kuhojiwa kwa zaidi ya saa sita kabla ya kwenda kumfanyia upekuzi na kurudishwa kituoni saa nne usiku na kubaki kituoni mpaka leo asubuhi kwa ajili ya maamuzi mengine.

 

Hii ni taarifa rasmi kuhusu sakata hilo.

MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI CUF TAIFA MHE. JULIUS MTATIRO YUPO NGANGARI;

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA UMMA

Imetolewa leo Tarehe 5 July,2018
Na. Kurugenzi ya Habari –CUF Taifa

Jana Tarehe 4/7/2018 Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi Taifa Mhe. Julius Mtatiro alipokea simu ya wito wa kuhitajika kituo Cha Polisi (Central Police) Dar es Salaam.

Leo Tarehe 5/7/2018 Mhe. Julius alikuwa amealikwa kama Mmoja wa Wageni wawezeshaji wa mjadala na Taasisi ya Twaweza katika Kongamano la kujadili MAONI YA WANANCHI KUHUSU USHIRIKI, MAANDAMANO NA SIASA lillilopangwa kufanyika katika kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere International Convention Centre –JNICC. Ilipofika saa 3 asubuhi akiwa anaelekea huko alipigiwa simu kujulishwa afike kituoni hapo saa 4 asubuhi.

Niliambatana nae (Maharagande) mpaka kituoni hapo na tulipokelewa na ZCO na kujulishwa kuwa anahitajika achukuliwe maelezo yake kuhusu ujumbe aliotuma katika ukurasa wake wa facebook unaosema “RAIS KITU GANI BWANA”. Tukakabidhiwa Maafisa wa Polisi wa kufanya kazi hiyo. Wakati wa kuanza kuchukuliwa maelezo yake alielezwa kuwa anatuhumiwa kwa “ KUTUMA UJUMBE WA KUJELI NA KASHFA DHIDI YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA” kupitia mtandao wa kijamii. Mhe Julius amechukuliwa maelezo yake mpaka saa 10 jioni na baadae kuelekea nyumbani kwake kwa upekuzi na kurejea tena kituoni majira ya saa 4 usiku. Maafisa wa polisi wameeleza kuwa wataendelea kuwa nae mpaka kesho asubuhi na kutujulisha kama watampatia dhamana au vinginevyo.

Mwisho:

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi Taifa Mhe. Julius mtatiro anawataka wanachama wa CUF kujitokeza kwa wingi Mahakamani kushuhudia Hoja makini zitakazotolewa na Mheshimiwa Bashange. Na wala wasiwe na hofu yeyote juu yake kwani yupo NGANGARI SANA. Shukrani kwa Msomi Wakili Hashimu Mziray kwa kusimamia vyema mahojiano hayo, Bakari Kasubi –Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mzimuni, Shaweji Mketo-Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi CUF Taifa, Anderson Ndambo na Kassimu Chogamawano[maafisa wa Kurugenzi ya Habari Taifa] kwa Uratibu wenu wa suala hili mpaka saa 5 za usiku huu.

HAKIKA TUPO VIZURI SANA, MAPAMBANO YA KISHERIA YANAENDELEA NA HAKI ITASHINDA.

HAKI SAWA KWA WOTE

MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI
NA MAHUSIANO NA UMMA-TAIFA.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari za Siasa

Dk. Biteko aipongeza NMB kwa kuanzisha utoaji wa bima ya mifugo

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!