Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mufti Zubeir: Hakuna hijja
Habari Mchanganyiko

Mufti Zubeir: Hakuna hijja

Aboubakar Zubeir, Mufti wa Tanzania
Spread the love

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), limesema mwaka huu hakutakuwa na ibada ya Hijja, kutokana na janga la Virusi vya Corona. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi tarehe 25 Juni 2020 na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir Ally wakati anazungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Mufti Zubeir amesema, hatua hiyo imetokana na zuio lililotolewa na nchi ya Saudi Arabia, kwa waumini wa Dini ya Kiislamu kutoka nje ya nchi hiyo, kufanya ibada hiyo, ili kudhibiti maambukizi ya Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu, inayosababishwa na Virusi vya corona (Covid-19).

Sambamba na hilo, Mufti Zubeir ameagiza madrasa zote nchini kufungulia kuanzia leo, huku akiwataka viongozi wa madrasa hizo, kufuata taratibu zote za kiafya, kwa ajili ya kujikinga na Covid-19.

Agizo hilo la kufunguliwa kwa madrasa, limekuja baada ya Rais John Magufuli, kuagiza shule zote nchini, kufunguliwa kuanzia Jumatatu ya tarehe 29 Juni 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!