Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mil. 780 zawaponza watatu Temesa, Majaliwa atoa maagizo mazito
Habari za Siasa

Mil. 780 zawaponza watatu Temesa, Majaliwa atoa maagizo mazito

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu,
Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa Sh. 780 milioni zinazotokana na zabuni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Pia, Majaliwa ametoa muda wa miezi miwili kwa taasisi zote za Serikali zinazodaiwa na TEMESA kiasi cha Sh. 25.88 bilioni ziwe zimeshalipa na iwapo kuna taasisi itashindwa kulipa deni lake hadi tarehe 30 Julai, 2020 apewe taarifa.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo Jumanne trehe 19, Mei, 2020 alipotembelea karakana ya mitambo ya TEMESA jijini Dodoma na amewasisitiza watumishi hao wafanye kazi kwa uadilifu na Serikali haihitaji wala haitowavumilia watumishi wazembe.

Watumishi waliosimamishwa kazi ni Mkurugenzi wa Huduma Saidizi, Hans Lyimo, Kaimu Mhasibu Mkuu, Jonas Bakuza na Lecian Mgeta aliyekuwa Mhasibu wa Wakala huo ambaye aliandika barua ya kuacha kazi tarehe 6 Aprili 2020.

Majaliwa ameagiza mtumishi huo arudishwe kazini ili akajibu tuhuma zinazomkabili.

“Kazi hii imefanywa kwa ushirikiano na Afisa wa benki ya CRDB asiyekuwa muaminifu ambaye naye tutamtafuta hadi tumpate.”

“Fedha hizo zilikuwa kwenye mfumo wa hundi wao wakazibadilisha na kuziweka katika mfumo wa fedha taslimu. Umakini usipokuwepo fedha zote zitakuwa zinaliwa tu,” amesema Majaliwa.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu amemuonya Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Japhet Maselle kutokana na usimamizi wake usioridhisha, ambapo amesema Mtendaji huyo alikuwa anajua kuhusu upotevu wa fedha katika wakala huo na hakuchukua hatua kwa wahusika.

“…si mzuri kwenye usimamizi unapenda kuacha watu wanaofanya maovu wakiwemo na watumishi hawa watatu. Mtendaji ulikuwa unajua, ulikuwa hauchukui hatua hadi uliposikia nakuja, hii si sahihi sheria zipo na maelekezo ya Serikali yapo. Upotevu wa Sh.780 milioni katika taasisi ni doa.”

Waziri Mkuu amesema kufuatia na matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa TEMESA, amemuagiza Mdhibiti na Makaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akafanye ukaguzi katika wakala huo kutokana na upotevu wa Sh.780 milioni zilizotakiwa zipelekwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amezitaka taasisi zote za Serikali zinazodaiwa na wakala huo ziwe zimelipa madeni yote katika kipindi cha miezi miwili ili kuiwezsha TEMESA kuweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

“Tukishapata bilioni 25 TEMESA hii tukapeleka walau bilioni moja moja kila mkoa watanunua mitambo, watanunua vipuri na magari yatatengenezwa kwa haraka. Magari yote ya Serikali lazima yatengenezwe TEMESA kwa sababu ya uhakika wa usalama wake,” amesema Majaliwa

Pia, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa wakala huo ufanye maboresho makubwa kiutendaji ikiwa ni pamoja na kufanya marekebisho ya sehemu ya magari kwa kuwa inalalamikiwa zaidi hususani suala la utengenezaji wa magari yanayopelekwa.

Waziri Mkuu amesema Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa wanalalamikia gharama kubwa wanazotozwa kwa ajili ya utengenezaji wa magari, hivyo lazima ziangaliwe kama ni halisi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa wakala huo ujiridhishe kila kivuko kama ni kizima ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kutokea na wavifanyie ukaguzi wa mara kwa mara.

Awali, Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Maselle alisema wakala huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo madeni makubwa yanayotokana na huduma zao kutolipwa kwa wakati au kutolipwa kabisa.

“…kwa mfano hadi mwezi Machi 2020 tunazidai taasisi za Serikali kiasi cha shilingi 25,882,593,038 na wakati huo huo tukidaiwa na wazabuni mbalimbali kiasi cha shilingi 18,959,630,408.”

Changamoto nyingine aliyoitaja ni uchakavu wa karakara nyingi zinazomilikiwa na wakala huo katika makao makuu ya mikoa mbalimbali nchini, hivyo kuathiri ufanisi katika matengenezo ya magari ya Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!