Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe afichua kitakachoiua CCM
Habari za SiasaTangulizi

Membe afichua kitakachoiua CCM

Spread the love

BERNARD Membe, mgomeba urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, ametaja kitachoiua Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, sumu kubwa iliyopandwa na chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020, ni mpasuko ndani ya chama hicho.

Membe ametoa kauli hiyo leo Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020 katika uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya ACT-Wazalendo, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Membe aliyekuwa waziti wa mambo ya nje kuanzia mwaka 2007 hadi 2015 enzi za utawal wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kiwkete amesema, ndani ya CCM kuna mpasuko baina ya kundi la wanachama wapya na wa zamani.

Membe ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali katika uzinduzo huo, lililohoji kama vyama vya upinzani vitaweza kuing’oa CCM madarakani kupitia uchaguzi huo.

“Kama unadhani CCM iko kitu kimoja na hakutakuwa na sauti za malalamiko ndani ya CCM za kusema tumechoka, sawa lakini ukweli ni kwamba CCM imegawanyika kati ya wale wa zamani na wapya, waliotumbuliwa na kutumbua,” amesema Membe.

Akijibu kauli ya Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM kwamba chama hicho ‘kinatesti mitambo,’ ACT-Wazalendo haitesti bali ipo mzigoni.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk. Bashiru Ally

“Bashiru nisikilize huko uliko, tunakusubiri kwenye majukwaa, sisi hatu-test mitambo, sisi tunaitekeleza, hatui-test tunaiwasha,” amesema Membe, mwanadiplomasia mashuhuri nchini.

Membe ameeleza kuumizwa na hatua ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea wa vyama vya upinzani.

“Nimeshiriki chaguzi sita, sijawahi kuona vituko vya mwaka huu, hii ni mpya ningekuwa na maneno ya kuazima ningesema huu ni uchaguzi wa ajabu, haujawahi kutokea hata gender (jinsia) mnaiengua?

“Binti yangu mwanamke anaacha Viti Maalum anakwenda kupambana na wanaume, mnamuengua? Usawa wa kijinsia uko wapi? Ndio maana sisi tukija tutakuja na gender balance (uswa wa kijinsia),” amesema Membe.

Mgombea huyo wa urais amesema, tatizo sio CCM bali tatizo ni baadhi ya watu wanaotumia vibaya madaraka yao.

“Nitapata nafasi nzuri kesho Lindi kuifafanua na kuichambua ilani yetu na kesho nitasema tatizo kubwa sio CCM.”

“Tatizo kubwa ni watawala wanaotumia vyombo vibaya na hivyo kusababisha matatizo makubwa ya kuhatarisha usalama wa Taifa letu,” amesema Membe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!