MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), imetangaza ukosefu wa maji kwa saa 24 kwa wakazi wa maeneo ya Vigwaza hadi Buyuni Mji wa Chalinze mkoani Pwani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi tarehe 30, 2020 na Ofisi ya Mawasiliano ya Dawasa imesema huduma hiyo itakosekana kuanzia leo hadi kesho Jumapili tarehe 31 Mei, 2020.
Katika taarifa hiyo imeeleza, sababu ya ukosefu wa majisafi ni kuhamisha bomba ili kupisha upanuzi wa barabara katika eneo la Mizani ya magari Vigwaza.
Maeneo yatakayoathirika ni Vigwaza, Visezi na Buyuni. Dawasa imewaomba radhi wananchi wa maneno hayo kwa kwa usumbufu utakaojitokeza.
Leave a comment