Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lwakatare kutinga CUF, kupokelewa na Prof. Lipumba
Habari za Siasa

Lwakatare kutinga CUF, kupokelewa na Prof. Lipumba

Wilfred Lwakatare, Mbunge wa Bukoba Mjini
Spread the love

WILFRED Lwakatare, Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anatarajiwa kurejea kwenye chama chake cha awali cha CUF. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Leo Jumamosi tarehe 30 Mei 2020, Lwakatare anatinga katika Ofisi Kuu za Chama cha Wananchi (CUF), zilizoko Buguruni jijini Dar es Salaam, na atapokelewa na Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho.

Safari ya Lwakatare kutinga katika ofisi za CUF, imeanzia kwenye ofisi za Tawi la CUF la Kosovo, lililoko katika Kata ya Manzese Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Lwakatare alikuwa muasisi wa tawi hilo la CUF, wakati akiwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, kabla hajajiunga na Chadema.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya CUF, leoLwakatare anakabidhiwa kadi ya chama hicho na Prof. Lipumba.

Hatua ya Lwakatare kutinga CUF, ambako aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, imetokana na uamuzi wa Chadema, kumvua uanachama, kwa tuhuma za kukiuka sheria za chama hicho.

Lwakatare aliondolewa Chadema, kufuatia hatua yake ya kugoma kutii maelekezo ya chama hicho, ya kujiweka karantini kwa muda wa siku 14, ili kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19.)

Agizo hilo liliwataka wabunge wa Chadema kutohudhuria vikao vya bunge kuanzia tarehe 3 hadi 17 Mei mwaka huu, lakini Lwakatare na wenzake 16, walikaidi na kuhudhuria bungeni.

Pamoja na kuunda kambi rasmi ya mpito, ya upinzani bungeni, huku Lwakatare akichaguliwa kuwa kiongozi wake.

Hata hivyo, hatua ya Lwakatare kurejea CUF inakinzana na tamko lake alilolitoa katika nyakati tofauti, ikiwemo bungeni, la kustaafu shughuli za siasa.

Hivi karibuni wakati anatangaza kutogombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba 2020, bungeni jijini Dodoma, Lwakatare alisema hatoshiriki tena shughuli za siasa, na wala hatajiunga na chama chochote.

Jana tarehe 29 Mei 2020, Mwanahalisi Online ilipopata taarifa za Lwakatare kurejea CUF, ilimtafuta kwa njia ya simu juu ya ufafanuzi wake, lakini alikana kwa kusema  hana mpango wa kurudi katika chama hicho.

Lwakatare alisema, anakwenda CUF kwa kuwa alipata mualiko, ambao ni sehemu ya heshima ya chama hicho kwake,  kutokana na  mchango wake katika ujenzi wa taasisi hiyo.

“Mimi msimamo wangu uko palepale, sina mpango wa kujiunga na chama chochote, nimestaafu siasa. Lakini ninaendelea kutoa ushauri kwa chama kama kinahitaji. Na mimi ni miongoni mwa watu waliokijenga CUF, hivyo sitakubali kife au kipoteze ushawishi,” amesema Lwakatare na kuongeza:

“Nitaendelea kukishauri juu ya namna bora ya kuwa chama chenye kuaminika kwa umma na  imara.”

Licha ya kauli hiyo kutoka kwa Lwakatare, kuna tetesi ya kwamba huenda akagombea tena katika Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CUF.

Mohammed Chapa, Katibu wa CUF katika Tawi la Kosovo, jana aliuambia mtandao huu kuwa, kuna uwezekano wa Lwakatare kugombea tena jimbo hilo.

Chasa alidai kuwa, Lwakatare ameshafanya mazungumzo na viongozi wa CUF katika jimbo lake, kuhusu suala hilo.

Hata hivyo, Chasa alisema kama Lwakatare hatogombea, CUF itamtumia katika mikakati yake ya ushindi kwenye jimbo la Bukoba Mjini, katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!