Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama yawabwaga wapinzani kesi ya muswada
Habari za Siasa

Mahakama yawabwaga wapinzani kesi ya muswada

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Tanzania imetulia mbali shauri la kupinga Muswada Sheria ya Vyama vya siasa iliyonguliwa na Zitto Kabwe, Salumu Biman na Joran Bashange. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Zitto ambaye ni Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Biman Mkuregenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Wananchi (CUF) na Bashange Naibu Katibu (CUF)Bara.

Viongozi hao waliowakili vyama 10 vya upinzani walifungua shauri hilo kupinga muswada wa sheria hiyo usijadiliwe bungeni kupitia jopo la Mawakili wao walioongozwa na Mpoki Mpare.

Leo Jaji Benhajo Masoud ametoa uamuzi huo, amekubali hoja za mawakili wa serikali kuwa Bunge ni muhimili unaojitegemea na haupaswi kuingiliwa na Mahakama.

Wiki iliyopita Jaji Masoud alisikiliza hoja za Serikali zilizotaka shauri hilo lifutiwe mbali kwa sababu zilizodaiwa na Mawakili wa Serikali kuwa Mahakama haiwezi kuingia mamlaka ya Bunge.

Moja ya hoja zilizowasilishwa na serikali kuwa Katiba ya Nchi imegawa mamlaka na kuyaheshimu.

Akiongoza jopo la Mawakili, Wakili Mkuu wa Serikali Mark Mulwambo alieleza kuwa Mahakama haiwezi kuingilia Muhimili wa Bunge katika kujadilia mambo yake.

Wakili ameeleza kuwa mahakama inaweza kujadili sheria iliyotungwa na Bunge siyo muswada ambao haujapitishwa kuwa sheria.

Hoja nyingine ya Serikali ni kwamba waombaji wamewasilisha maombi yao kwa kiapo chenye udhaifu ambao hakuna mahala kinapoeeleza muombaji namba moja Zitto.

Kiapo hiko hakina iaini ya Zitto ambapo kina upungufu ambapo kimeambatanisha saini ya waombaji wawili tu ambapo wametaka kwa udhaifu huo kesi hiyo iondelewe mahakamani hapo.

“Muswada siyo sheria mpaka usainiwe ndiyo uweze kuwa sheria kwa sasa Bunge liachwe lifanye kazi yake kisheria na kwamba huo muswada haupo kwenye Ofisi ya Waziri mkuu wala Ofisi ya Mwanasheria Huu Muswada upo bungeni,” alieleza.

Alieleza kuwa wabunge wanauwezo wa kutoa maoni ya marekebisho bungeni kwa kuwawakilisha wananchi.

Upande wa watoa maomba uliongozwa na Wakili Mpare Mpoki umekitaka kifungu cha ibara ya 5 kwenye katiba inayoipa mahakama mamlaka ya kutengea sheria au hatua yoyote itakayochukuliwa na Serikali au Mamlaka yoyote kwa kukiuka haki, uhuru na wajibu kama ilivyoanisha ibara ya 12 hadi 29 kwenye katiba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Askofu Bagonza: CDF Mabeyo amepasua masikio yetu

Spread the loveMJADALA kuhusu safari ya mwisho ya maisha ya Hayati Rais...

Habari za Siasa

10 matatani kwa kutorosha madini ya bil 1.5

Spread the loveJeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Kikosi...

Habari za Siasa

Wagombea 127 wa udiwani kutoka vyama 18 kuchaguliwa kesho

Spread the loveWagombea udiwani 127 kutoka vyama 18 vya siasa wanatarajiwa kupigiwa...

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

error: Content is protected !!