Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif amgomea Zitto
Habari za Siasa

Maalim Seif amgomea Zitto

Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, mgombea urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo, amekataa ombi la Kiongozi wa chama hicho, Zitto Zuberi Kabwe la kurudi nyumbani baada ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 27 na 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Zitto alitoa ombi hilo jana Jumapili tarehe 13 Septemba 2020 katika mkutano mkubwa wa uzinduzi wa kampeni za urais visiwani humo, uliofanyika Uwanja wa Demokrasia – Kibanda Maiti, Unguja.

Kiongozi huyo alisema, wamejipanga kuhakikisha vijana wa chama hicho wanalinda kura na baada ya kutangazwa kwa matokeo, watamfuata Maalim Seif nyumbani kumpeleka Ikulu.

“Oktoba 28, baada ya kura, tutaomba Maalim Seif, uende nyumbani ukapumzike, tutakufuata sisi nyumbani kwako tukupeleke Ikulu baada ya kazi ya kulinda ushindi wetu.”

“Sisi vijana wako tutaifanya hiyo Kazi,” alisema Zitto huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.

Zitto alisema “ngoma itakavyopigwa ndivyo tutakavyoicheza, tumefuata sheria, wametunyang’anya haki zetu.”

“Kuna mambo sio ya Muungano, lakini yamepokwa na Tanganyika kupitia Muungano. Michezo si jambo la Muungano, kwanini Zanzibar si Mwanachama wa FIFA.”

“Watoto si Jambo la Muungano, kwanini Zanzibar haipo UNICEF? ACT-Wazalendo tutaipa Zanzibar haki hizo inazominywa,” alisema Zitto

Zitto ambaye pia ni mgombea ubunge wa Kigoma Mjini alisema “Zanzibar haitaki kusaidiwa, Zanzibar inataka iendeshe uchumi wake yenyewe.”

“Zanzibar haipaswi kusaidiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inapaswa kupewa haki yake. Shelisheli nchi ya Kisiwa kama Zanzibar, Ina watu 80,000 tu, wanasaidiwa na Nani?”

Baada ya Zitto kumaliza kuzungumza, Maalim Seif alipanda jukwaani. Pamoja na mambo mengine aliyozungumzia, aligusia ombi la Zitto la kumtaka kupiga kura na kurejea nyumbani.

 

“Kiongozi wa chama kaniomba nikishakupiga kura, nikatulie nyumbani, eti nikajifiche. Namtaka radhi, nasema NO! Wakifanya hujuma nitatoka na nitaongoza mapambano ya kuitetea nchi yangu.”

“Nitakuwa mstari wa mbele, na kama kufa basi nife mimi mwanzo. Sawa Sawa,” aliuliza na kujibiwa ndiyooooo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!