Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli ajibu wanaohoji maendeleo Chato
Habari za Siasa

Magufuli ajibu wanaohoji maendeleo Chato

Hayati John Magufuli, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Spread the love

JOHN Magufuli, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema, wanaohoji kwa nini amejenga Uwanja wa Ndege Chato mkoani Geita “washindwe na walegee.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwandishi Wetu … (endelea).

Rais Magufuli amesema, Serikali ya awamu ya tano anayoingoza imepeleka maendeleo nchi nzima lakini baadhi ya watu wamekuwa wakihoji kwa nini Chato.

Chato mkoani Geita ndiko nyumbani kwao, Rais Magufuli.

Hayo ameyasema leo Jumatatu tarehe 14 Septemba 2020, wakati akihutubia umati wa wananchi kwenye mkutano wa kampeni za urais katika Uwanja wa Mazaina, Chato mkaoni Geita.

Amesema, kila kijiji nchini Tanzania, Serikali yake imetekeleza miradi ya maendeleo, ikiwemo miundombinu ya barabara, madaraja, upanuzi wa bandari na vituo vya afya.

“Mtu anazungumza eti nimejenga uwanja wa Ndege nyumbani, nikifa nitaenda nalo hilo liuwanja kaburini!?, lazima upange mipango mipana, tumejenga viwanja zaidi ya 11 huko Singida, Songea, Mtwara,Dodoma lakini hivyo vyote hawavioni wanakiona cha Chato tu tena  washindwe na wakalegee,” amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.

Amesema “mtu anasimama ameshiba ugali anasema ndege hazina faida, yeye alipotoka huko alikuja na Bajaji?, angetoka huko alipotoka na Bajaji mpaka hapa? unajua mambo mengine yanakera.”

Rais Magufuli amewaomba Watanzania kumchagua tena ili akamilishe kipindi chake cha pili cha miaka mitano (2020 – 2025).

“Tunaomba miaka mingine mitano haya maajabu tutayafanya kweli, kila mkoa, kijiji kuna tulichofanya, Dar es Salaam kuna barabara za juu hakuna mtu aliyetegemea. Hatukufanya tu masuala ya viwanda, tumepanua bandari zetu, tumenunua Meli Nyasa,”  amesema.

Kiongozi huyo wa nchi amesema, katika uongozi wake amefanikiwa kupunguza changamoto ya uhaba wa madarasa, kutoa elimu bure kuanzia Shule ya Msingi hadi Sekondari.

“Hapa Chato shule zilikuwa hazitoshi, madarasa hayakuwepo, sekondari hazikuwepo ndio maana tulipoingia madarakani awamu ya tano tulisema, lazima tuweke mikakati kuhakikisha watoto wetu wanaenda shule ili kuhakikisha wengi wanaenda shuleni, ndio maana tulifuata ada,” amesema Rais Magufuli.

Pia, amesema, Serikali yake imeongeza idadi ya vijiji vilivyounganishwa umeme kutoka 2,011 vya awali hadi 9700 kati ya vijiji vyote 1,228 nchi nzima, ameahidi endapo akichaguliwa tena, vijiji 2,500 vilivyosalia ataweka umeme ndani ya miaka mwili.

“Nchi yetu hii wakati tunaingia madarakani (5 Novemba 2015) kulikuwa na watumishi hewa zaidi ya 20,000 wanalipwa mishahara wakati si watumishi, tulifuta majina hewa tukaajiri watu halisi, miaka mitano tuliajiri wafanyakazi zaidi ya 80,000,” amesema Rais Magufuli.

1 Comment

  • Pemba kapeleka maendeleo gani ama pemba sio sehemu ya tanzania. Ama wapemba wanastahili kuuliwa tu na sio maendeleo?Tunaona hivi sasa majeshi yote na polisi wa Bara wanaletwa pemba kosa letu ni nini ama kosa ni kuikataa CCM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!