Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu azidi kuruka vihunzi kugombea urais Tanzania
Habari za SiasaTangulizi

Lissu azidi kuruka vihunzi kugombea urais Tanzania

Spread the love

MKUTANO Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania, umemteua Tundu Antipus Lissu, kuwa mgombea urais wa nchi hiyo utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia, mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam leo Jumanne tarehe 4 Agosti 2020, umemteua Salum Mwalimu kuwa mgombea mwenza wa urais.

Mkutano mkuu huo wenye wajumbe 1001, umepitisha mapendekezo ya Baraza Kuu la Chadema ambalo jana Jumatatu lilimpendekeza Lissu kwa kura 405 sawa na asilimia 91 ya kura zote 442 zilizopigwa na wajumbe.

Lazaro Nyalandu alipata kura 36 na Dk. Mayrose Majinge akiambulia kura moja kwenye mbio hizo za kumpata mgombea mmoja. Wote kwa pamoja walikubali matokeo hayo na kusema wako tayari kuungana na Lissu na chama kuhakikisha wanashinda uchaguzi mkuu.

Kuteuliwa kwa Lisuu, kunamfanya kwenda kuchuana na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Pombe Magufuli ambaye naye tarehe 11 Julai 2020, alithibitishwa na chama hicho kuwa mgombea urais.

Rais Magufuli atakuwa anatafuta fursa ya kuongoza Watanzania katika muhula wa pili na wa mwisho Kikatiba wa miaka kumi. Aliingia Ikulu kwa mara ya kwanza tarehe 5 Novemba 2015.

Pia, Mohamed ikiwa atagombea urais wa Zanzibar, atakwenda kuumana na wagombea wa vyama vingine akiwemo Maalim Seif Sharif Hamad wa ACT-Wazalendo na Dk. Hussein Ali Mwinyi wa CCM.

Awali, Mwalimu akizungumza na wajumbe wa mkutano huo kabla ya kumteua amesema, katika kipindi chote amekuwa mwaminifu kwa chama kwa kufanya kazi mbalimbali.
“Tumekisimamisha chama chetu Zanzibar tofauti na miaka mingine nyuma. Katika operesheni ya Chadema ni msingi, ndani ya miezi 18 nimekanyanga majimbo yote nchini,” amesema.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema

Mwalimu ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari amesema, anakwenda kuwa mgombea mwenza anayeijua nchi yote “na mgombea wetu Tundu Lissu ajue ana mgombea wa aina gani anayekwenda kufanya naye kazi.”

Lissu: Siwezi kuenguliwa

Akizungumza na wajumbe wa mkutano huo, Lissu amesema, “mkutano mkuu huu unamfahamu Tundu Antipus Lissu na wengi wengi kama siyo wote, mmewahi kuniona au kunisikia nikifanya kazi sehemu mbalimbali, sidhani kama mimi nahitaji kutambulishwa kwa mkutano mkuu huu.”

Lissu amegusia suala la yeye kuenguliwa katika uchaguzi huo ambapo akiwaonyesha fomu ya mapingamizi amesema, “hii hofu ya kuenguliwa. Fomu za pingamizi wanaotaka kuniwekea na kuna sababu 16.”

“Katika sababu zote 16 wanazotaka kuniwekea, hakuna hata moja inayonihusu mimi. Kwa hiyo, kama wanapanga pingamizi, litakuwa nila kihuni tu,” amesema Lissu huku wajumbe wakimshambulia.

“Masharti yaliyopo hapa, hakuna linalonikaribia hata moja. Nasikia sikia ile fomu ya maadili ya umma, ili hilo litimie linapaswa nihukumiwe na baraza la maadili ya umma.”

“Lakini inabidi nishtakiwe kwanza, niambiwe nijitetea, nishindwe kesi kisha baraza la maadili liseme wew0e umeshindwa. Sasa sijawahi kushtakiwa,” amesema Lissu.

Amesema, kitendo cha kupoteza ubunge wa Singida Mashariki kwa kigezo cha kutokujaza fomu za maadili ya viongozi wa umma hakukifanya kwa sababu alikuwa hospitalini akijiuguza.

“ Wabunge wote mliopo humu ndani, mliletewa, mimi nililetewa wapi. Nilikuwa hospitalini, sikuletewa na nilikuwa nataka kufa. Kwa sababu hawakuniletea, hawajanishtaki wala kuhukumiwa na kama wanataka kuniwekea mapingamizi ya kihuni, wafanye lakini tunasema sasa basi,” amesema.

Katika kugusia hilo, Lissu ambaye kitaaluma ni mwanasheria amesema, “hivi nani aliyesema kwamba, wao hawawezi kuwekewa mapingamizi? Kwamba mapingamizi ni ya wapinzani peke yake? Nani amesema?”

Kitendo hicho kiliufanya mkutano huo kushangilia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!