Dk. Helen Kijo Bisimba

Kijo-Bisimba ataja athari wabunge wengi CCM

Spread the love

USHINDI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  katika ngazi ya ubunge katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano ya tarehe 28 Oktoba 2020, umetajwa kwenda kuathiri majukumu ya Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Hadi kufikia saa 9 alasiri ya leo Ijumaa tarehe 30 Oktoba 2020, Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) CCM imejinyakulia majimbo 220 kati ya 264 huku upinzani wakipata viti viwili pekee.

Hali hiyo, ni tofauti na Uchaguzi Mkuu uliopita mwaka 2015 ambapo kati ya wabunge 264, upinzani ilikuwa na majimbo zaidi ya 65.

Kati ya wabunge wa vili maalum na wale wa majimbo, CCM ilikuwa na wabunge 272, Chadema 71, ACT-Wazalendo na NCCR-Mageuzi kila kimoja kikipata mbunge mmoja.

Vyovyote itakavyokuwa, katika Bunge la 12 linalotarajiwa kuitishwa Novemba 2020, CCM kitakuwa na wabunge wengi zaidi huenda kuvuka robo tatu ya wabunge wote.

Hali hiyo inamfanya Dk. Helen Kijo-Bisimba, Mkurugenzi Mstaafu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) kusema, uchache wa wabunge wa upinzani bungeni, utasababisha sauti mbadala kukosekana bungeni.

bunge la tanzania

“Mfumo  wa vyama vingi unasaidia kuweka watu walioko nje ya Serikali kwa ajili ya kuangalia kasoro zake, majukumu yao  kuona mambo yanaendaje, kama nchi kutakuwa na Serikali haina wa kuwatazama watafanya wanachotaka,” amesema Dk. Bisimba alipokuwa anazungumza na MwanaHALISI ONLINE.

Dk. Bisimba amesema, “hii italeta athari kwa wananchi ambapo upinzani walikuwa wanaoneshe mambo ya rushwa, wapinzani walikuwa wanaibua hayo mambo ya kimaendeleo ambayo kwa sasa hawataibua.”

Amesema, kazi ya upinzani bungeni ni kuisimamia Serikali iliyoko madarakani pamoja na kuikosoa inapokwenda kinyume, kitendo ambacho ni nadra kufanywa na wabunge wa CCM.

“Bunge lijalo hakutakuwa na kuwajibisha Serikali sababu Bunge litakuwa la chama kimoja, kama wananchi watakosa pa kuzungumzia kwa kuwa Bunge ni sehemu ya wananchi kutoa matatizo,” amesema Dk. Bisimba.

Ukumbi wa Bunge

Kuhusu mahusiano ya kimataifa, Dk. Bisimba amesema, yatayumba kwa kuwa dunia iliizoea Tanzania yenye mfumo wa vyama vingi ambao unawawakilishi katika vyombo vya maamuzi.

“Kuhusu mahusiano ya kimataifa bahati mbaya, hakukuwa na waangalizi wa kutosha, nchi za nje wameutazamaje uchaguzi huu, kama wataona kuna kasoro wataona shida, wataona hatujakomaa kidemokrasia na kuleta shida katika mahusiano,” amesema Dk. Bisimba.

Dk. Bisimba amesema, “nchi zote zinazungumzia umuhimu nchi kuendesha mambo yao kidemokrasia, sasa kuna shida kimahusiano na nchi ambazo sisi wanachama wa kimataifa.”

Mtetezi huyo wa haki za binadamu amevishauri vyama vya upinzani kujipanga upya na kuangalia namna ya kuihami demokrasia nchini.

“Vyama vya upinzani, waangalie kama wanaweza kujifunga upya, kama miaka iliyopita walikabwa na waliendelea kufanya kazi zao, kwa hiyo visikate tama.”

“Wale wanaopenda mageuzi waendelee wasikate tama, waendelee kwa njia mbalimbali, wakiona demokrasia ya uchaguzi imetushinda watafute mbinu nyingine,” ameshauri Dk. Bisimba.

USHINDI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  katika ngazi ya ubunge katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano ya tarehe 28 Oktoba 2020, umetajwa kwenda kuathiri majukumu ya Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea). Hadi kufikia saa 9 alasiri ya leo Ijumaa tarehe 30 Oktoba 2020, Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) CCM imejinyakulia majimbo 220 kati ya 264 huku upinzani wakipata viti viwili pekee. Hali hiyo, ni tofauti na Uchaguzi Mkuu uliopita mwaka 2015 ambapo kati ya wabunge 264, upinzani ilikuwa na majimbo zaidi ya 65. Kati ya wabunge wa vili maalum na wale wa majimbo, CCM ilikuwa na wabunge…

Review Overview

User Rating: 2.78 ( 2 votes)

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!