BAO lililofungwa katika dakika ya 87 na Theo Walcott, mchezaji wa Klabu ya Everton katika mechi ya Ligi Kuu Uingereza (EPL), limezamisha ndoto ya mchezi wa kimataifa wa Tanzania anayechezea Klabu ya Aston Villa, Mbwana Samatta kubaki EPL msimu ujao. Inaripoti mtanda wa habari wa BBC…(endelea).
Walcott ameongeza mzigo kwa Samatta na klabu yake kwamba, ili iweze kucheza EPL, basi klabu hiyo inapaswa kushinda mechi zake mbili zilizosalia kati yake na Arsenal pia West Ham, vinginevyo msimu ujao watausikia kwenye bomba.
Villa ambayo ilikuwa ugenini, ilipigana kufa kupona ili itoke na ushindi na hatimaye kuinua manumaini ya kubaki EPL msimu ujao, bao la Ezri Konsa katika uwanja wa Everton – Goodison Park – liliongeza ari kwa Villa.
Kwa sasa Villa ipo katika nafasi ya 19 EPL, ina pointi nne nyuma ya Watford, ambayo inashikilia nafasi ya mwisho juu ya eneo la kushushwa daraja.
Arsenal ambayo hivi karibuni iliwatandika mabingwa Liverpool, inaonekana kuimarika huku wakiwa na matumaini ya kushinda mechi mbili zilizosalia ikiwemo ya Aston Villa.
West ham ambayo ipo katika nafasi ya 16 na haijacheza mechi moja, iko pointi sawa na Watford na inatishiwa kushuka daraja iwapo itapoteza mechi tatu zilizosalia.
Mashabiki wa Villa pia watakuwa wakiangalia matokeo ya klabu ya Bounemouth, Watford na West Ham katika wiki zijazo.
Leave a comment