Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Biashara ya ngono yamwibua Lugola
Habari Mchanganyiko

Biashara ya ngono yamwibua Lugola

Spread the love

WATU wanaosafirisha watoto wa kike kutoka mikoa mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kufanya biashara ya ngoni, waonywa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ametoa onyo hilo leo tarehe 30 Julai 2019, wakati akihutubia katika maadhimisho ya siku ya kupinga baishara haramu ya usafirishaji binadamu, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Lugola amesema, waathirika wakubwa wa biashara hiyo ni watoto wadogo wa kike wenye umri kuanzia miaka 13 hadi 24, ambapo wengi wao hutolewa maeneo ya vijijini na kuletwa mjini.

“Biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu hapa nchini inayoongoza ni ya kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine, waathirika ni watoto wadogo, wasichana na vijana ambao wako katika umri wa miaka 13 hadi 24,” amesema Lugola.

Lugola amesema, Jiji la Dar es Salaam linaongoza kwa biashara haramu ya usafirishaji binadamu, likifuatiwa na Tanga na Dodoma.                                                     

“Watu wanasafirishwa nje kwa kuahidiwa kazi nzuri, wengi wanatokea la Dar es Salaam, Tanga na Dodoma, waathirika ni wanawake wenye miaka 16 – 26, ingekuwa ni kuku umri huu tungewaita mtetea kwa sababu wakifika kule wanafanya biashara ya ukahaba,” amesema Lugola.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!