April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli uso kwa uso na Mbowe msibani

Rais John Magufuli alipohani msiba wa Meja Jenerali Alfred Mbowe nyumbani kwake Salasala, Dar es Salaam

Spread the love

RAIS John Magufuli leo tarehe 30 Julai 2019 ametoa salamu za pole kwa familia ya marehemu Meja Jenerali Mstaafu, Alfred Mbowe, aliyefariki dunia tarehe 28 Julai mwaka huu. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Rais Magufuli ametoa salamu hizo alipowasili nyumbani kwa marehemu Jenerali Mbowe, maeneo ya Salasala jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli alipokelewa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa ambaye ni mdogo wa marehemu Meja Jen. Mstaafu Mbowe.

“Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Salasala jijini Dar es Salaam. Kutoa pole kwa familia kufuatia kifo cha Meja Jen. Mstaafu Alfred Lameck Mbowe,” inaeleza taarifa ya Msigwa.

error: Content is protected !!