Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yafanyia mabadiliko Katiba yake
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yafanyia mabadiliko Katiba yake

Spread the love

MKUTANO Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, umefanya marekebisho ya Katiba ya chama hicho. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mabadiliko hayo yamefanyika jana Jumatano tarehe 5 Agosti, 2020 katika mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa ACT-Wazalendo, Omary Said Shaban, Katiba hiyo itabadilishwa katika mambo mawili yaliyopo kwenye Ibara ya 42 na 79 A ibara ndogo ya pili.

“Mapendekezo ni mawili, pendekezo la kwanza linagusa Ibara ya 42 ya Katiba na Ibara ya 79 A ibara ndogo ya pili, ” amesema Shaban.

Kabla ya mabadiliko ya Katiba hiyo kufanyika, Shaban amesema ACT-Wazalendo imeamua kufanya mabadiliko ya Ibara ya 42 inayotoa maelekezo juu ya uongozi wa majimbo, kwa kuwa uongozi huo umeathirika baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar-ZEC kufuta majimbo manne visiwani humo.

Hivyo, mabadiliko hayo yanalenga kuwezesha uchaguzi mpya wa uongozi katika majimbo yaliyoathirika.

“Ndugu wajumbe Ibara ya 42 kama inavyosomeka kwa sasa inahusu majimbo kwa maana uongozi ACT-Wazalendo ngazi ya majimbo.

“Inasomeka bila kuathiri masharti ibara ndogo ya kwanza, ambapo tume imetangaza mabaidliko ya majimbo ya uchaguzi na kuathiri uongozi wa ACT- Wazalendo, marekebisho yanapendekeza  sekretarieti ya chama kuagiza kuitishwa uchaguzi kwenye majimbo kwa mujibu wa tangazo la ZEC,” amesema Shaban.

Shaban amesema, mabadiliko hayo ya ZEC kwenye majimbo, yameathiri mchakato wa kura za maoni kutafuta wagimbea wa majimbo husika.

“Athari ya mabadikilo hayo  mkutano mkuu wa jimbo ambao ulikuwa na mamlaka kufanya kura za maoni. Katika kurekebisha katiba tumeona vyema kupendekeza kwenu basi sekretarieti kuitisha uchaguzi wa majimbo yaliyoathirika kwa mujibu wa tanangazo la ZEC,” amesema Shaban.

Kuhusu mabadiliko ya Ibara ya 79 (2), yamelenga kuipa mamlaka Kamati ya Uongozi ya ACT-Wazalendo kuchagua mtu atakayeshika nafasi ya Makamo wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Shaban amesema kwa sasa  katiba ya chama hicho inatoa mamlaka kwa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu kufanya uteuzi huo, jambo ambalo litachelewesha chama hicho kuteua makamo wa rais wa SMZ kwani mchakato wa kuitisha vikao hivyo ni wa muda mrefu sana.

“Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar uteuzi wa makamo wa rais unafanyika ndani ya siku 7 kutoka tarehe aliyoapishwa rais mteule, kutokana na urahisi wa vyombo kukutana ni rahisi kuitisha kamati ya uongozi kuliko kamati kuu na halmashauri kuu ya chama,” amesema Shaban.

Kufuatia mabadiliko hayo, kama Kamati ya Uongozi ACT-Wazalendo itateua Makamu wa Rais wa Kwanza wa SMZ, badala ya Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu wa chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!