Saturday , 18 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Jafo azindua kitabu cha maarifa ya utunzaji mazingira
Habari Mchanganyiko

Waziri Jafo azindua kitabu cha maarifa ya utunzaji mazingira

Spread the love

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk. Seleman Jafo amezindua Kitabu cha Maarifa ya Asili katika Uhifadhi wa Mazingira , Misitu na Vyanzo Maji kilichoandaliwa na Taasisi ya Wanahabari ya Kusaidia Jamii za Pembezoni (MAIPAC) kwa kushirikiana na Taasisi ya CILAO. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea)

Kitabu hicho kimetokana na simulizi za wazee wa mila ya kimasai, wanawake na vijana wa jamii hizo katika wilaya za Ngorongoro, Longido na Monduli.

Akizindua kitabu hicho jana Februari 11 mwaka huu jijini Arusha, Waziri Jafo amepongeza MAIPAC kwa kuja na mradi huo wa aina yake na kueleza serikali itawaunga mkono.

“Huu ni mradi wa kwanza wa aina yake nawapongeza MAIPAC kwa kazi nzuri kwani pia nimeona makala nzuri na nina imani Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na wafadhili wengine wataendelea kuwapa fedha zaidi kuendeleza mradi huu,”amesema

Amesema uhifadhi wa mazingira kwa maarifa ya asili ni muhimu, kwani maarifa hayo yalikuwa yanatumika toka enzi za mababu ambapo imesaidia kutunza misitu, vyanzo vya maji na mazingira na kitabu hicho kitakuwa njia sahihi ya kueneza elimu ya utunzaji wa mazingira kwa njia ya asili.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa MAIPAC, Mussa Juma, amesema kuwa kitabu hicho kimeelezea simulizi za jamii ya masai wanavyotumia taratibu na mila zao katika kutunza mazingira, vyanzo vya maji na misitu.

Amesema mradi huu ulizinduliwa rasmi Agosti 27,2022 na umefadhiliwa na Programu ya Miradi Midogo ya Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF) unaotekelezwa na UNDP nchini Tanzania chini ya uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais –Idara ya Mazingira.

Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa Arusha, Blandina Nkini ameipongeza MAIPAC kwa kuwa shirika pekee lililokuja na mradi wa uhifadhi wa mazingira kwa kutumia maarifa ya asili na kuwa moja ya shirika la mfano mkoani Arusha kati ya mashirika 1,114 yaliyosajiliwa mkoani Arusha na kuwaomba wafadhili wengine kuwasaidia katika kutekeleza miradi yao.

Mratibu wa Miradi Midogo UNDP, kupitia Shirika la GEF, Faustine Ninga ameipongeza MAIPAC kwa kukamilisha kuchapa vitabu na kuandaa video na machapisho ya mradi huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

error: Content is protected !!