Sunday , 7 July 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri alia siasa kushamiri matukio manane ya utekaji 2024
Habari za SiasaTangulizi

Waziri alia siasa kushamiri matukio manane ya utekaji 2024

Spread the love

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema katika kipindi cha mwaka huu kuanzia Januari kumetokea matukio manane ya utekaji na asilimia kubwa ya watuhumiwa wa utekaji huo wamekamatwa na kufikishwa mahakamani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza katika uzinduzi wa kitabu cha Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar  Zubeir ameeleza kushangazwa na siasa kuingizwa katika mtukio hayo kwa kuyahusisha na vyombo vya dola ambavyo jukumu lake ni kulinda raia na mali zao.

Amesisitiza kuwa vyombo vya usalama vina uwezo wa kutosha kukamata watuhumiwa wote wa utekaji na kudhibiti matukio hayo.

Hamad Yusuf Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania

Masauni ametoa kauli hiyo wakati Tanzania ikizizima kuhusu tukio la utekaji alilofanyiwa kijana Edgar Mwakabela, maarufu kama Sativa anayedaiwa kutekwa, kuteswa na kutupwa katika pori la Hifadhi ya Katavi akiwa na majeraha mbalimbali mwilini.

Sativa ambaye anaendelea na matibabu katika hospitali ya Aga Khan kuanzia usiku wa tarehe 30 Juni mwaka huu, alidaiwa kutoweka tarehe 23 Juni mwaka huu na kupatikana tarehe 27 Juni mwaka huu katika pori hilo.

Hata hivyo, alipopatikana Sativa anadai alitekwa na watu wasiojulikana na kupelekwa kwenye karakana iliyopo Kituo cha Polisi Oysterbay Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kupelekwa Katavi.

Tyari Rais Samia Suluhu Hassan amesema yeye binafsi atabeba gharama zote za matibabu yake pamoja na uchunguzi wa tukio hilo.

Matukio mengine ni pamoja na Mtoto Albino Asimwe Novart aliyeuawa Wilayani Muleba Mkoani Kagera Mei mwaka huu kabla ya mwili wakekupatikana Juni.

Hata hivyo, watuhumiwa tisa akiwamo baba yake tayari wamekamatwa wakiwa na viungo vya mtoto huyo wakitafuta Mteja mkoani Kagera.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mwabukusi aenguliwa Urais TLS, mwenyewe agoma

Spread the loveKAMATI ya Rufaa ya Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), imemuengua...

Habari za SiasaKimataifa

Starmer atangaza baraza jipya la mawaziri UK

Spread the loveKufuatia ushindi wa kishindo ambao chama cha Labour kimeupata katika...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Bodi ya sukari, wazalishaji jino kwa jino

Spread the loveMVUTANO wa utoaji wa vibali za sukari na nakisi umeendelea...

error: Content is protected !!