Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Wabunge Marekani waguswa uhifadhi Ngorongoro
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wabunge Marekani waguswa uhifadhi Ngorongoro

Spread the love

Wabunge wa Bunge la Wawakilishi la Congress kutoka nchini Marekani wamepongeza juhudi za uhifadhi zinazofanywa na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro hususan utunzaji na ulinzi wa wanyamapori adimu kama faru wakiwa katika maeneo yao ya asili.  Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Maliasili kutoka bunge hilo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Arkansas, Bruce Westernman na wabunge wenzie wametembelea maeneo mbalimbali ikiwepo hifadhi ya Ngorongoro kupata uzoefu wa shughuli za uhifadhi za nchi zingine na namna unavyochangia kuvutia watalii na kuona jinsi sera za uhifadhi za USA zinavyoweza kuchangia athari chanya kwa uhifadhi na utalii wa bara la Afrika.

“Timu yetu tunafanya ziara hii kama sehemu ya mafunzo ya kuiona juhudi za uhifadhi kwa nchi za Afrika ikiwemo Ngorongoro na kuona namna gani sera za Marekeni zinaweza kuwa na ushirikiano chanya  kwenye sekta ya uhifadhi na Utalii kwa hifadhi za bara la Afrika” ameeleza Westernman.

Wabunge hao wamefurahishwa kuona namna uhifadhi endelevu ulivyoongeza idadi ya wanyamapori mbalimbali ikiwemo wanyama wakubwa watano ambao ni faru, simba, chui, tembo na nyati ambapo wabunge hao walifanikiwa kuwaona ndani ya muda mfupi katika hifadhi hiyo.

Naye, Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA Dk. Elirehema Doriye ameeleza ujumbe wa wabunge hao kuwa, Serikali kupitia NCAA imeendelea kuhakikisha kuwa vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro vinaalindwa, kutunzwa, kuhifadhiwa sambamba na kuibua mazao mapya ya utalii kwa ajili ya kuvutia wageni wa mataifa mbalimbali wanaotembelea eneo hilo kwa shughuli za utalii, utafiti na elimu ya masuala ya uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori na utunzaji wa mazingira.

Naibu Kamishna wa Uhifadhi (Uhifadhi, Utalii na maendeleo ya Jamii), Vicktoria Shayo ameeleza ujumbe huo kuwa pamoja na juhudi za uhifadhi katika eneo la Ngorongoro kumeliwezesha eneo hilo kupata hadhi tatu za kimataifa zinazotambuliwa na UNESCO ambazo ni tabaka hai la kimataifa (Biosphere Reserve), Urithi mchanganyiko wenye historia ya binadamu katika eneo la Olduvai na Laetoli (Mixed worl heritage site) na eneo lenye sifa ya utalii wa miamba na Jiolojia (Ngorongoro Lengai UNESCO Global Geopark).

Kwa upande wake Afisa Utalii mkuu wa NCAA Peter Makutian ameeleza ujumbe kuwa eneo la hifadhi ya Ngorongoro lina vivutio vingi na vya kipekee ikiwemo Wanyama wa aina mbalimbali, kreta za Ngorongoro, Olmoti, Empakai, makumbusho ya Olduvai na Marry Leakey, mchanga unaohama, tambarare za ndutu, mlima olmoti ambao ni wa tatu kwa urefu Tanzania na kuongeza kuwa ujumla wa vivutio hivyo umeiwezesha eneo la hifadhi ya Ngorongoro kuwa kivutio bora cha utalii barani Afrika 2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!