Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Vifo vya wanaokufa maji vyafikia zaidi ya laki 2, EMEDO watoa neno
Habari Mchanganyiko

Vifo vya wanaokufa maji vyafikia zaidi ya laki 2, EMEDO watoa neno

Spread the love

 

SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la usimamizi wa Mazingira na Maendeleo ya Uchumi (EMEDO) limesema kuwa takwimu za shirika la afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa zaidi ya watu Mia mbili kwa mwaka wanakufa kutokakana na kuzama maji. Anaripoti, Erasto Masalu, Dar es Salaam … (endelea). 

Hayo yamesemwa Juni 4,2024 na Mkurugenzi wa Shirika hilo Editruda Lukanga wakati wa warsha ya siku moja ya wanahabari na wadau mbalimbali wa masuala ya Hali ya hewa ikiwemo Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) na kusema kuwa kuna haja ya kushirikiana kwa pamoja ili kutoa elimu ambayo itasaidia kuzuia watu hasa wavuvi kufa maji.

Amesema katika ripoti hiyo ya WHO inaonyesha asilimia 90 ya vifo hivyo vinatokea katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hivyo ni wakati muafaka sasa kwa nchi kuchukua hatua hususani katika kipindi hiki ambacho mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa yakitokea.

Amesema kuwa wapo baadhi ya watu wanakufa maji kutokana na uzembe hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari ya maji yatokanayo na mvua kubwa, mito, maziwa na bahari kwani kwa kuwa yanaua na kuacha simanzi kwa familia, jamii na Taifa Kwa ujumla.

“Ni wakati sasa wa kuleta mabadiriko na kuchangia usalama wa namna tunavyotumia maji”. Amesema

Kwa upande wake, Ofisa uhusiano wa TMA, Monica Mutoni amesema wanashirikiana vema na shirika hilo la EMEDO na wadau wengine ili kuzuia watu kupata na changamoto mbaya za mabadiliko ya Hali ya hewa ukizingatia kuwa watu wanaofanya shughuli zao katika maziwa makuu na ukanda wa bahari wanakumbana na athari za Hali mbaya ya hewa hususani upepo mkali.

“Kama mnavyofahamu TMA sisi jukumu letu kutoa taarifa za hali ya hewa na moja ya jukumu letu ni kutoa taarifa za hali ya hewa upande wa sekta ya uvavi tunashirikiana na wenzetu Imedo kuhakikisha kuwa taarifa hizo zinawafikia wavavi” alisema.

“Wenzetu wanaofanya shughuli zao kwenye ukanda wa bahari na maziwa makuu wanapata changamoto nyingi kutokana athari za hali ya hewa hususani upepo mkali na sisi TMA tumetoa tabiri za msimu wa Juni mpaka Agosti kuwa kitakuwa kipindi cha kipupwe kutakuwa na upepo mkali kwa baadhi ya siku ambazo tutakuwa tukitoa taarifa hivyo upepo huo utaleta athari upande wa bahari na maziwa kwa hiyo tutashirikiana na wenzetu kuhakikisha zinawafikia wahusika kwa wakati na kuchukua hatua stahiki”

Amesema kuwa TMA itaendelea kutoa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa vipindi vya kila siku kwa lengo la kuokoa mali na maisha ya wananchi.

Naye Meneja Mradi wa kuzuia kuzama maji Ziwa Viktoria Arthur Mugema amewashauri watu wanatumia bahari, mito na maziwa wakiwemo wavuvi kuhakikisha wanakuwa na vifaa maalumu vya kuogelea kama vile mambo ya okozi ( life Jacket) na kuwafanya wasizame maji pindi vyombo wanavyotumia vinapopata hitilafu na kuiomba Serikali kuona umuhimu wa kupunguza gharama za vifaa hivyo.

Amesema, mwaka 2021 walifanya utafiti wa kwanini kuna ajari nyingi za wavuvi kuzama ziwani na mtazamo wa wavuvi, jamii na viongozi kule chini pamoja na madhala wanayopata familia ambayo imempoteza mtu wanayemtegemee.

Amesema kuwa katika utafiti wao waligundua kuwa wavuvi wana uelewa hafifu juu ya matumizi ya vifaa vya uokoaji na hawapati taarifa za hali ya hewa kwa wakati.

“Tulibaini kuwa wavuvi wanauelewa mdogo kwenye elemu ya usalama kwe ye Mji , matumizi ya vifaa maboya okozi wavuvi wachache wanaovaa ijapokuwa sheria inawataka wavae,…. changamoto nyingine ni upatikanaji wa maboya okozi pamoja na gharama zake zimekuwa kubwa. ” alisema.


Amesema, baada ya kubaini changamoto hizo ndipo wakaja ma mradi mradi wenye lengo la kupunguza ajali za wavuvi kuzama katika Ziwa Victoria mradi ambao unatekelezwa kanda ya Ziwa katika Mikoa ya Mwanza, Kagera na Mara.

“Mradi huu ulioanza mwakan 2022 mpaka 2025 tukilenga kuwabadilisha wavuvi mtazamo na kutoa elimu juu ya matumizi ya maboya okozi ambapo mpaka sasa tumekwisha anza kutengeneza maboya okozi yatakayowawezesha wavuvu kukaa muda mrefu kwenye maji”

Ameiomba serikali kupunguza kodi ya uingizaji vifaa hivyo ili vipatikane kirahisi ili kupunguza ajali hizo.

Amesema kuwa lengo kubwa la mradi huo ni kusapoti maendeleo ya uchumi wa Bluu kwa kuwa usalama wa nguvu kazi ya utendaji huo.

Aidha ameeleza kuwa mbali na kutoa elimu kwa wavuvi wanatoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari zilizoko katika Maeneo yaliyoko Kanda ya Ziwa Kwa kuwa walengwa wakubwa ni wavuvi, watoto na akina mama wachakatani wa samaki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

Habari Mchanganyiko

Sangoma awaponza vijeba, watupwa jela maisha kwa kubaka wanafunzi

Spread the loveMAHAKAMA ya wilaya Nkasi Mkoani Rukwa, imemhukumu kifungo cha maisha...

error: Content is protected !!