Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura 147 ili kuelekeza asilimia mbili ya mapato ya ushuru wa bidhaa yanayokusanywa kutoka kwenye bidhaa za urembo, vinywaji laini na vileo (bia na pombe kali) kwenye bima ya afya kwa wote.
Amesema lengo la hatua hiyo ni kuongeza fedha zitakazotumika kwa ajili ya kugharamia bima ya afya kwa watu wasio na uwezo na makundi maalum hususan wanawake wajawazito na watoto wa umri chini ya miaka mitano.
Akiwasilisha bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/2025, amesema hatua hiyo inatarajia kupeleka kiasi cha Sh 18.8 bilioni katika mfuko mkuu wa serikali.
Leave a comment