Sunday , 30 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sababu Diane kung’olewa uchaguzi Rwanda zatajwa
Habari za SiasaKimataifa

Sababu Diane kung’olewa uchaguzi Rwanda zatajwa

Diane Rwigara
Spread the love

Mkuu wa Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Rwanda, Oda Gasinzigwa amesema jina la Diane Rwigara (42) ambaye ni kiongozi wa vuguvugu la People Salvation halijapitishwa katika kinyang’anyiro cha wagombea urais nchini humo kwa sababu ameshindwa kutoa hati inayothibitisha kuwa ana asili ya Rwanda. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).

Pia amesema mwanamama huyo ambaye katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 pia alikataliwa kugombea urais, ameshindwa kuwasilisha taarifa ya rekodi ya uhalifu kama inavyoagizwa na tume ya uchaguzi na badala yake akatoa nakala ya hukumu ya mahakama.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mkuu huyo wa tume pia ameongeza kuwa; “Kuhusu sharti la kupata uidhinishaji wa saini za watu 600, hakutoa angalau saini 12 kutoka wilaya nane.”

Rwigara alikataliwa kugombea mwaka 2017 kwa tuhuma za kughushi saini za wafuasi wake kwa ajili ya fomu yake.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 42 alikamatwa, na kushtakiwa kwa kughushi na kuchochea uasi na kufungwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kuachiliwa huru mwaka 2018.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame atakabiliana na wapinzani wawili katika uchaguzi wa mwezi ujao, kulingana na orodha ya muda ya wagombea urais iliyochapishwa jana Alhamisi.

Gasinzigwa amewataja Kagame, Frank Habineza wa chama cha Democratic Green Party na mgombea huru Philippe Mpayimana kama wagombea katika uchaguzi wa tarehe 15 Julai mwaka huu.

Wote Habineza na Mpayimana walikuwa pia wagombea pekee walioruhusiwa kushindana na Kagame katika uchaguzi wa mwaka 2017.

Gasinzigwa alisema katika tangazo kwenye televisheni ya serikali kwamba jumla ya fomu tisa za wagombea watarajiwa zilipokelewa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Tanzania yakubali kukutana na mabalozi 9 kutatua changamoto za kikodi

Spread the loveSerikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na...

error: Content is protected !!