Tuesday , 2 July 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania yaiuzia Zambia mahindi tani 650,000
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Tanzania yaiuzia Zambia mahindi tani 650,000

Mahindi
Spread the love

Tanzania imeuza mahindi tani 650,000 nchini Zambia ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kufuatia mazungumzo kati ya Rais Samia Suluhu na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema tarehe 26 Aprili mwaka huu na kufuatiwa na mazungumzo kati ya wizara za kisekta na balozi za nchi hizi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ambapo amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuwa msaada kwa washirika wake wakati wa uhitaji.

Zambia imeingia makubaliano ya kununua mahindi kutoka Tanzania ili kusaidia wananchi wake zaidi ya milioni saba wanaokabiliwa na njaa kutokana na ukame ulioikumba nchi hiyo.

Mbali na kuwasaidia raia wa Zambia kupata chakula wakati huu wa uhitaji, pamoja na kuimarisha uhusiano, udugu na ushirikiano baina ya nchi hizi, makubaliano hayo yanayotekelezwa kwa kipindi cha miezi nane yataiingizia Tanzania Sh 650 bilioni.

January Makamba

Zaidi ya hekari milioni moja ziliathiriwa na ukame nchini Zambia pamoja na mvua za El Nino na hivyo kuiweka nchi hiyo katika uhitaji mkubwa wa chakula ili kunusuru maisha ya wananchi wake.

Tanzania na Zambia ni marafiki wa muda mrefu katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika ambapo ushirikiano wao ulianza tangu wakati wa kupigania uhuru chini ya waasisi wa mataifa haya Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Kenneth Kaunda. Udugu huu wa miaka na mikaka unathibitishwa na miradi ya uwili kama Boma la Mafuta la Tanzania na Zambia (TAZAMA) pamoja na Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Tofauti kati ya Rais Ruto, Naibu wake zaanikwa

Spread the loveTOFAUTI za kimtizamo kati ya Rais William Ruto na Naibu...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Maandamano yaibuka upya Kenya

Spread the loveVIJANA wa Kenya waliojipachika jina la Generation Z (Gen Z)...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

TRA yaweka rekodi makusanyo 2024, yakusanya trilioni 27.64

Spread the loveWAKATI wafanyabiashara nchini wakiweka mgomo wa siku tatu kupinga makadirio...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NSSF yawataka wastaafu watarajiwa kuhakiki taarifa zao

Spread the loveMfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) umewataka watumishi...

error: Content is protected !!