Sunday , 23 June 2024
Home Kitengo Biashara Tanesco yawasha mtambo namba 8 Bwawa Julius Nyerere
BiasharaHabari za Siasa

Tanesco yawasha mtambo namba 8 Bwawa Julius Nyerere

Spread the love

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amesema tayari mtambo namba nane kutoka kwenye Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere umekamilika na sasa unaingiza megawati 230 kwenye gridi ya taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Dk. Biteko ametoa taarifa hiyo jana Ijumaa wakati akizindua taarifa za utendaji katika Sekta ndogo ya Umeme, Gesi Asilia na Mafuta kwa mwaka 2022/2023 jijini Dodoma.

Amesema kwa sasa jumla ya megawati 470 zinazalishwa kutoka JNHPP na tayari zimeingizwa kwenye gridi ya taifa.

Kuhusu sekta binafsi amesema, “Sekta binafsi imetutoa kimasomaso, Serikali haiwezi kufanya kila kitu, wamefanya kazi kubwa mno kwenye mafuta, gesi na hata kwenye uzalishaji umeme, wito wangu kwenu msibaki nyuma changamkieni fursa, na kwa taasisi zilizo chini ya Wizara msione sekta binafsi kama watu wajanjawajanja, tuwape kipaumbele.”

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kuwa katika tathmini iliyozinduliwa inaonesha Sekta ya Nishati  imepiga hatua kwenye maeneo mengi ikiwemo uhakika wa upatikanaji umeme, upatikanaji na usambazaji wa mafuta kuimarika hasa baada ya Dk. Biteko kuanza kuongoza Wizara ya Nishati.

Ameongeza kuwa, taarifa ya Benki ya Dunia kwa nchi za dunia ya tatu zinazofadhiliwa na Benki hiyo inaonesha kuwa sekta ya nishati kwa Tanzania inafanya vizuri zaidi katika nchi zote zinazoendelea na Bara la Afrika kwa ujumla.

Amesema hayo ni matunda ya usimamizi madhubuti wa Dk. Biteko ambapo eneo lililofanya vizuri zaidi ni usambazaji umeme vijijini na miradi mingine ya nishati kama JNHPP na mradi wa TAZA.

Ameongeza kuwa Benki ya Dunia imeidhinisha Dola za Marekani milioni 300 ili ziendeleze sekta ya umeme kutokana na ufanisi huo wa Tanzania.

Akitoa taarifa za utendaji katika sekta ya nishati, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Andilile alisema kuwa sekta ya nishati inaendelea kuimarika ikiwemo uwekezaji kwenye miundombinu ya

umeme uwekezaji umeongezeka katika uzalishaji, usafirishaji na usambazaji.

Amesema upotevu wa umeme unazidi kupungua na kubainisha wateja wa umeme wameongezeka kutoka milioni 3.8 mwaka 2021/22 hadi milioni 4.4 mwaka 2022/2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Kibaha na Meridianbet waendeleza ushirikiano

Spread the love Meridianbet wameendelea kua na ushirikiano na wakazi waKibaha kwani...

Biashara

Meridianbet kasino inatoa mgao wa Tsh 2,500,000/= leo 

Spread the love  Cheza na Ushinde bonasi ya kasino kupitia michezo mingi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washiriki mbio za NBC Dodoma Marathon kutumia treni ya SGR kwenda Dodoma

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

error: Content is protected !!