Sunday , 30 June 2024
Home Kitengo Biashara Taifa gesi yaja na mitungi ya bei nafuu kwa wanafunzi vyuo vikuu
BiasharaHabari Mchanganyiko

Taifa gesi yaja na mitungi ya bei nafuu kwa wanafunzi vyuo vikuu

Spread the love

Kampuni ya kuuza nishati ya gesi ya kupikia majumbani ya Taifa Gas Limited imezindua mpango wake maalum unaotoa punguzo la bei ya nishati hiyo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ikiwa ni muendelezo wa jitihada za kampuni hiyo kufanikisha adhma ya serikali inayolenga kuhakikisha asilimia 80 ya wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hafla ya uzinduzi wa program hiyo ilifanyika jana Jumatano eneo la Changanyikeni, Wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiambatana na uzinduzi wa duka maalum litakalowahudumia wanafunzi hao kwa punguzo hilo la bei. Kuashiria uzinduzi huo jumla ya mitungi ya gesi 300 ilitolewa bure kwa baadhi ya wanafunzi hao na wakazi wa maeneo jirani ili kuchochea hamasa ya mpango huo.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule (wa nne kulia) akikabidhi moja kati ya mitungi ya gesi 300 iliyotolewa bure na Taifa Gas Limited kwa baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Dar es Salaam na wakazi wa eneo Changanyikeni wilayani Kinondoni.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule aliongoza hafla hiyo iliyohudhiriwa na wawakilishi wa wanafunzi na uongozi wa vyuo kutoka vyuo vikuu mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Takwimu, Chuo cha Ardhi na Chuo cha Maji. Meneja Mauzo wa Taifa Gas, Joseph Nzumbi alimuwakilisha Meneja Mkuu wa Taifa Gas, Devis Deogratius kwenye uzinduzi huo.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huduma hiyo, DC Mtambule alisema huduma hiyo imekuja wakati muafaka kipindi ambacho serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan inapambana kuhakikisha inafanya kila liwezekanalo kuwasaidia na kuwawezesha wananchi  kupitia makundi yao mbalimbali kuifikia nishati hiyo kwa urahisi.

“Ni faraja kubwa zaidi kwetu kama serikali kuona kwamba wakati tunaendelea kufanikisha mkakati wa kufikia nishati safi ifikapo 2034 tayari wadau kama Taifa Gas wameanza kubuni mbinu mbalimbali za kijamii na kimasoko zitakazotusaidia kama taifa kufanikisha adhma hiyo. Kupitia huduma hii ya punguzo la bei kwenye kila mtungi wa gesi wanafunzi wa vyuo vikuu watavutiwa zaidi na kuona matumizi ya gesi kama suluhisho sahihi la nishati ya kupikia…hongereni sana Taifa Gas,’’ alipongeza.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule (mbele katikati) akiwa kwenye picha pamoja na wawakilishi wa wanafunzi na uongozi wa vyuo kutoka vyuo vikuu mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Takwimu, Chuo cha Ardhi na Chuo cha Maji na wananchi wa eneo la Changanyikeni, Wilaya ya Kinondoni wakati wa hafla hiyo.

Awali akifafanua kuhusu mpango huo, Nzumbi alisema unahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Dar es Salaam wenye vitambulisho halali ambao watapata mapunguzo tofauti kulingana na uzito wa mitungi ya gesi watakayonunua.

“Kwa mfano bei ya kujaza mtungi wa gesi wenye uzito wa kg 6 badala ya wanafunzi kuuziwa kwa Tsh 23,000 kupitia mpango huu watauziwa kwa Tsh 20,000 na kwenye mtungi wenye uzito wa kg 15 wanafunzi watajaziwa gesi kwa Tsh 50,000 badala ya Tsh 55,000. Tumeanza na Dar es Salaam na tutaendelea kwenye vyuo vingine zaidi maeneo mengine,’’ alitaja.

Zaidi, akiwasilisha salamu za Meneja Mkuu wa Taifa Gas, Devis Deogratius, Nzumbi alisema kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha kwamba kila Mtanzania mwenye nia ya kutumia nishati safi ya gesi anapata fursa hiyo kupitia mikakati mbalimbali inayoendelea kubuniwa na kampuni hiyo kwa kuzingatia mahitaji ya makundi tofauti ya kijamii.

Wakizungumzia program hiyo, wadau na wanufaika wakiwemo wakiwemo wakuu wa vitivo, wawakilishi wa wanafunzi na wakazi wa eneo la Changanyikeni waliipongeza wakibainisha kuwa itaongeza chachu kwa wanafunzi hao kutumia zaidi nishati ya gesi badala ya mkaa kutokana na punguzo bei ambalo ndio kiini cha mpango huo.

“Wanafunzi ni kundi ambalo bado halijaanza kujitengenezea kipato chao wao wenyewe hivyo wapo makini sana na masuala ya bei ya bidhaa wanazotumia hususani kwa wale wanaojipikia kwenye maeneo yao. Ujio wa mpango huu wa punguzo la bei ya mitungi ya Taifa Gas utakuwa kimbilio kwao ili waweze kuokoa fedha zao. Nawaomba sana wanafunzi waichangamkie huduma hii,’’ alisisitiza Bw Wenslaus Richard, Mkuu wa Kitivo Msaidizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kauli iliyoungwa mkono na wanafunzi hao.

Hafla hiyo iliambatana na utoaji wa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitungi hiyo kwa wanufaika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Biashara

Cheza sloti za Expanse kasino! mamilioni yanakusubiri 

Spread the love  Leo ni zamu yako kushinda na kuibuka Mfalme wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!