Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Sukari pasua kichwa, wabunge wang’ang’ana wapiga dili watajwe
Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Sukari pasua kichwa, wabunge wang’ang’ana wapiga dili watajwe

Spread the love

SAKATA la sukari limeendelea kuwa mjadala mzito ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muunga wa Tanzania linaloendelea sasa huku baadhi ya wabunge wakimtaka Spika wa Bunge hilo, Dk. Tulia Ackson kuwataja mawaziri wanaopiga dili katika biashara hiyo na kuihujumu serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yameendelea kuibuka katika Bunge hilo la bajeti wakati wabunge na Watanzania wakisubiri taarifa ya ushahidi wa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kumhusu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe aliyemtuhumu kulidanganya Bunge namna alivyoshughuliki uhaba wa sukari nchini.

Wakichangia Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 leo bungeni jijini Dodoma, baadhi ya wabunge waliipongeza Serikali kwa kuhodhi uagizaji wa sukari kutoka nje.

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (CCM) amemuomba Spika Dk. Tulia kuwataja majina ya waziri anayedaiwa kupiga dili katika uagizaji huo wa sukari, lakini pia amtaje waziri anayedaiwa kumhujumu Bashe ili wananchi wafahamu ukweli.

“Hawa wote ni wateule wa Rais Samia, tunaomba suala hili lifanyiwe kazi. Pia tuambiwe faida ya kuleta sukari kutoka nje ni ipi na faida ya kuimarisha viwanda vya ndani ni ipi, lengo ni kwamba tusilishwe matango pori. Hili jambo ni muhimu… lisifanyiwe kampeni,” amesema Mwita.

Amesema sakata hilo la sukari linawachanganya akili wabunge, ilihali wananchi ambao ni walipa kodi, nao wakishindwa kuelewa kwanini viongozi ambao ni wateule wa rais wanafuja mali bila kuchukuliwa hatua.

Naye Mbunge viti Maalumu, Lucy Mayenga amesema suala hilo la uhaba wa sukari limekuwepo katika awamu mbalimbali za uongozi nchini mbali na Rais Samia.

Ameipongeza Serikali kwa kushughulikia sakata hilo katika kipindi hiki ambacho wafanyabiashara wachache walitaka kuishikilia nchi.

“Ninyi mawaziri zungumzeni lugha moja. Msipozungumza lugha moja huku nyuma mnatutesa sisi wengine,” amesema.

Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu (CCM) naye amesema sakata hilo limeendelea kuwa tete licha ya Serikali kuingilia kati na kuhodhi ununuzi wa sukari nje.

Amesema katika suala hilo, mpango wa Serikali kumiliki soko la sukari ndio jambo la msingi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lema: Nimesikitishwa na uamuzi wa Msigwa

Spread the loveMJUMBE wa Kamati Kuu Chadema, Godbless Lema ameeleza kushtushwa na...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Kura mbili zamhamishia Mch. Msigwa CCM

Spread the loveAliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini na mjumbe wa zamani wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Tanzania yaiuzia Zambia mahindi tani 650,000

Spread the loveTanzania imeuza mahindi tani 650,000 nchini Zambia ikiwa ni utekelezaji...

Habari za Siasa

Dk. Mpango, Ulega waongoza harambee ujenzi jengo la kitega uchumi CCM Pwani

Spread the loveMjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha...

error: Content is protected !!