SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba wameondoa kodi kwenye vifaa vya teknolojia ya usaidizi wa refarii kwa njia ya video (VAR) Katika mwaka wa fedha wa 2024/25. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Mwigulu ameyasema hayo wakati akiwasilisha bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/25 leo tarehe 13 Juni 2024 Bungeni jijini Dodoma.
Katika hotuba yake Mwigulu alisema kuwa msimu ujao wa mashindano wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/25, kumepangwa kutumia teknolojia hiyo katika michezo ya Ligi Kuu ili kuepesha sintofahamau na maamuzi ya utata.
Kwenye kutekeleza hilo kupitia makadilio ya bajeti hiyo, Mwigulu alisema kuwa msimu ujao Ligi Kuu itaanza matumizi ya VAR ili kuhakikisha maamuzi yanakuwa ya haki
“Spika, napenda kulifahamisha Bunge lako Tukufu kuwa, msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania tutaanza kutumia ”VAR” ili kuhakikisha matokeo yanayopatikana uwanjani yanakuwa ya haki maana kuna timu zimezidi – msimu mmoja penati 10, halafu zikifungwa zenyewe magoli yanakataliwa.”
“Na ili tuwe na ”VAR” za kutosha katika viwanja vyote, naleta pendekezo la kutoa msamaha kwenye uingizaji wa mashine za ”VAR” na vifaa vyake kwa ufafanuzi utakaotolewa hapo baadae. INAWEZEKANA!” alisema Mwigulu
Wakati Mwigulu akiwasilisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kwa sasa zipo kwenye maandalizi ya kuwa wenyeji wa michuano ya kombe la Mataifa Afrika (AFCON) 2027.
Katika Bajeti hiyo Serikali imepanga kukusanya na kutumia kiasi cha Shilingi 49.35 trilioni katika mwaka wa fedha wa 2024/25.
Leave a comment