Sunday , 7 July 2024
Home Kitengo Biashara NMB yakopesha bilioni 585 kwa mwaka 2023/2024
BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yakopesha bilioni 585 kwa mwaka 2023/2024

Spread the love

IMEELEZWA kuwa mazingira bora ya biashara yaliyopo nchini yameiwezesha Benki ya NMB kutoa mikopo ya zaidi ya Sh 585 bilioni katika kipindi cha kuanzia Julai 2023 hadi Mei 2024.

Pia benki hiyo imeeleza kuwa na uwezo wa kukopesha hadi Sh 515 bilioni kwa mkupuo mmoja ‘single borrower limit’ kutokana na kufanya vizuri kwenye soko la Tanzania Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yamebainishwa na Meneja wa NMB Tawi la Sabasaba, Kidawa Masoud katika banda la benki hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Tanzania ‘ sabasaba’ yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Kidawa amesema NMB inayo mizania wa zaidi ya Sh. 12.2 trilioni, jambo ambalo linaowahakikishia uimara na uwezo wa kukopesha hadi Sh. 515 bilioni.

Amesema uimara huo kiuchumi, unawapa uhakika wa kuendana na kasi ya Serikali, ambayo imeweka mazingira wezeshi kibiashara kama inavyoakisi kaulimbiu ya Maonesho ya Sabasaba mwaka huu isemayo; ‘Tanzania ni Sehemu Bora kwa Biashara na Uwekezaji.’

“Tuko imara kuhudumia kada zote za wateja wadogo, wa kati, wakubwa na mashirika ama kampuni, ambazo zinaweza kukopa kwetu hadi Sh 515 bilioni kwa mkupuo mmoja na nguvu hii inatokana na ongezeko la silimia 26 ya Faida Baada ya Kodi tuliyopata mwaka 2023 ya Sh. 542 bilioni.

“Mpango mkakati tulionao kwa ni kuwafikia Watanzania wengi zaidi kupitia mifumo ya kidijiti, ambayo imeonesha mafanikio makubwa sana, kwani asilimia 94 ya miamala iliyofanyika kwa mwaka jana, imefanywa nje ya matawi 231 ya benki yetu kote nchini.

“Katika kufanikisha hili, tunazo akaunti za NMB Pesa zinazofunguliwa kwa Sh. 1,000 tu, NMB Kikundi inayojumuisha wanachama wa vikundi mbalimbali vya kijamii, lakini pia tunao mkakati wa Huduma za Kibenki Vijijini ‘Rural Banking’ yenye lengo la kuvifikia vijiji 1,000 Tanzania,” alisema.

Kidawa alifafanua ya kwamba, ‘Rural Banking’ ni mkakati unaolenga kufungua akaunti milioni 1.5 kwa wakazi wa maeneo yasiyo na huduma za kibenki vijijini, kupitia mawakala wa benki hiyo waliotapakaa kila kona ya nchi.

Aidha, wakati kalenda ya Mwaka wa Fedha wa Serikali wa 2024/25 inayoanzia tarehe 1 Julai 2024 ikianza kutumika, NMB imetambia mafanikio katika makusanyo ya Mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzaibar (SMZ), ilikofanyia maboresho mifumo yao na serikali zote.

Kidawa amesema: “Mwaka huu tunaendeleza mashirikiano yetu na Serikali zote za Bara na Visiwani, katika kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato, ambako tumeweza kukusanya zaidi ya Sh. Trilioni 9.8 tangu mwaka 2018 kupitia NMB Wakala, NMB Mkononi na matawi yetu.”

Aliongeza ya kwamba, kama taasisi ya fedha kinara nchini, wanajivunia mafanikio yaliyowawezesha sio tu kutoa gawio kubwa zaidi la Sh. 57.3 bilioni kwa Serikali ya Tanzania ambayo inamiliki asilimia 31.8 ya Hisa za Benki ya NMB, bali kutwaa Tuzo ya Benki Bora Tanzania kwa mwaka wa 11 mfululizo.

“Ni mwaka ambao tulipata pia Tuzo ya Benki Bora Tanzania tuliyopewa na Jarida la Euromoney, lakini pia tukapata idhini ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana (CSMA), kuwa wakala wa madalali wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Banda la EACOP lawavutia wengi maonesho ya Sabasaba

Spread the loveWananchi na wadau mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kutembelea  Banda la...

Biashara

Shinda mamilioni kwa kucheza kasino na sloti ya Sticky 777

Spread the love  Moja kati ya biashara nzuri na yenye mtaji mdogo...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali yakanusha kuchelewa kutoa vibali vya uagizaji wa sukari

Spread the loveBODI ya Sukari Tanzania imekanusha taarifa za kuchelewa kutoa vibali...

error: Content is protected !!