Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko NGO’s kanda Magharibi zalia ukata, vitisho
Habari Mchanganyiko

NGO’s kanda Magharibi zalia ukata, vitisho

Spread the love

 

MASHIRIKA yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), yanayojishughulisha na masuala ya utetezi wa haki za binadamu, yameomba msaada wa kifedha kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).

Wito huo umetolewa jana Alhamisi, tarehe 18 Machi 2022, mkoani Kigoma, katika ziara ya Meneja Programu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Remmy Lema, kwenye mikoa ya Kanda ya Magharibi, iliyoanza tarehe 10 Machi mwaka huu.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mratibu wa THRDC Kanda ya Magharibi, Alex Luoga, amesema mshirika hayo yanakabiliwa na changamoto ya kifedha kutokana na kutokuwa na wafadhili wa kudumu na fedha za muda mrefu.

“Changamoto ya kifedha kwa wanachama wa kanda hii bado ipo, asasi nyingi hazina wafadhili wa kudumu na fedha za muda mrefu, wengi wanafanya kazi za kujitolea kwa nia ya kutoa huduma kwa jamii.

Changamoto hizi zimechangiwa na ujuzi mdogo wa uandishi wa miradi, iliyopelekea upatikanaji wa rasilimali fedha kuwa mdogo,” amesema Luoga.

Luoga ametaja changamoto nyingine zinazokabili mashirika hayo, ikiwemo ya kiusalama, kufuatia baadhi yake kupokea vitisho kutoka kwa jamii kutokana na kazi za utetezi wa haki za binadamu wanazozifanya, hasa kwa watoto, vijana na migogoro ya ndoa.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la CEDO, Japhet Kalegeya, ameiomba THRDC kuweka mikakati ya kuyajengea uwezo mashirika hayo katika kila kanda kwa kuwa changamoto zao zinafanana, huku akiiomba iyaunganishe na wafadhili.

“Mngetuwekea mkakati wa kutujengea uwezo na sit u kutujengea uwezo, bali na kutuunganisha na wafadhili, hapa tulikuwa na changamoto ya ukosefu wa wafadhili wa mara kwa mara, unaweza pata mfadhili akakupa ruzuku mara moja na akakata,” amesema Kalegeya na kuongeza:

“Na anapokata hana sababu za msingi za kukata, tuna ukosefu wa rasilimali fedha za mara kwa mara unakuta unamaliza miaka miwili hauna fedha.”

Akijibu changamoto hizo, Lemmy amesema THRDC itatafuta namna ya kushirikiana na wafadhili wa kitaifa na kimataifa, kuzitatua ikiwemo kupata fedha.

Akizungumzia ziara yake, Lemmy, amesema ametembelea mashirika 25, ambayo 17 ni wanachama wa THRDC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!