Tuesday , 2 July 2024
Home Habari Mchanganyiko Mgomo watikisa mikoa 8, wafanyabiashara wamuita Samia
Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mgomo watikisa mikoa 8, wafanyabiashara wamuita Samia

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana.
Spread the love

LICHA ya Rais Samia Suluhu Hassan kuahidi kuwa hadi kufikia tarehe 8 Agosti mwaka huu atakuwa ameinyoosha bandari ya Dar es Salaam na kuweka mazingira rafiki ya biashara, mgomo wa wafanyabiashara umeendelea kupamba moto katika mikoa nane. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mbali na Dar es Salaam ambayo mgomo huo umeingia siku ya tatu leo, mikoa ya Mtwara, Arusha, Mwanza, Songwe, Dodoma, Iringa na Mbeya nayo wafanyabiashara wake wametajwa kuanza mgomo kwa kufunga maduka yao.

Akizungumza na wafanyabiashara katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo Jumatano, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa amepigiwa simu na Rais Samia jana usiku na kumhakikishia ameagiza mfumo wa utozaji kodi urekebishwe.

“Nimeongea na Rais akasema mfumo ule ameagizwa urekebishwe haraka sana, Rais anawapenda Wafanyabiashara na alishatamka si mara moja anataka mazingira mazuri ya biashara, amemuagiza Kamishna Mkuu wa TRA mpaka tarehe 8 mwezi wa 8 pale Bandarini patakuwa pamenyooka.

“Nimepata simu ya Rais lakini bado siwalazimishi kuweni na amani hiyo hiyo, mimi niliomba nikamwambia Rais nakwenda kuwaambia wafanyabiashara haya tuliyozungumza na huu ndio utakua mkataba wetu.

“Wafanyabiashara wanataka walipe kodi zote kule kwenye kapu moja bandarini kama wanavyofanya waagizaji wa mafuta, sasa tuna maamuzi yetu binafsi kama Mwenyekiti nimezungumza hayo na Rais amenithibitishia sasa ni uamuzi wetu tuchague njia ya kuendea,” amesema Mwenyekiti huyo ambaye amewasisitiza kuwa wafanyabaishara hao ndio wenye uamuzi wa kufungua au kuendelea kufunga maduka yao.

Kauli hiyo ya Mwenyekiti wa wafanyabiashara Kariakoo imekusa saa chache baada ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo Jumatano, kukutana na kuzungumza na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.

Licha ya kwamba hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu kikao hicho, wafanyabiashara hao wameendelea kusisitiza kuwa wanataka kuonana na Rais Samia ili wazungumze naye ana kwa ana kutokana na kile wanachodai kutowaamini wasaidizi wake ambao wameshindwa kutatua changamoto zao.

Baadhi ya wafanyabiashara hao wamedai kuwa viongozi wao wamewapa mrejesho wa kero moja pekee ilihali wanazo kero nyingi ambazo zinapaswa kutafutiwa ufumbuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Tofauti kati ya Rais Ruto, Naibu wake zaanikwa

Spread the loveTOFAUTI za kimtizamo kati ya Rais William Ruto na Naibu...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Maandamano yaibuka upya Kenya

Spread the loveVIJANA wa Kenya waliojipachika jina la Generation Z (Gen Z)...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

TRA yaweka rekodi makusanyo 2024, yakusanya trilioni 27.64

Spread the loveWAKATI wafanyabiashara nchini wakiweka mgomo wa siku tatu kupinga makadirio...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NSSF yawataka wastaafu watarajiwa kuhakiki taarifa zao

Spread the loveMfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) umewataka watumishi...

error: Content is protected !!