Tuesday , 2 July 2024
Home Habari Mchanganyiko Mbowe: Tunawaunga mkono Kariakoo, mifumo ya kodi inaua mitaji
Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mbowe: Tunawaunga mkono Kariakoo, mifumo ya kodi inaua mitaji

Mbowe akihutubia Monduli
Spread the love

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema anawaunga mkono wafanyabiashara wa Kariakoo walioanza mgomo jana Jumatatu kuishinikiza serikali kutatua changamoto zao na kuwaomba wafanyabiashara wengine Tanzania nzima waungane na wenzao. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akihutubia wananchi na wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika Monduli jana, Mbowe amesema inabidi wafanyabiashara hao waungwe mkono ili serikali ijue namna wananchi walivyo na hasira kutokana na ugumu wa maisha.

“Wafanyabiashara wa Kariakoo wanasema kodi zimekuwa kubwa, wananchi wanashindwa kununua bidhaa, Serikali ipunguze kodi tunaua mitaji yetu. Tunawaunga mkono wafanyabiashara wa Kariakoo, tunawaomba wafanyabiashara wengine Tanzania nzima tufike mahali tuikatae hii Serikali ya wahuni,” amesema Mbowe na kuongeza;

“Hasira za namna hii ndio hicho watoto wa Kenya wanachofanya. Wakati tozo ya simu na miamala inaanzishwa, Watanzania tuliangalia lakini Wakenya wanajitambua wameandamana  mpaka serikali imekubali kuondoa.

“Hii mijamaa inakopa sana kwa sababu zaidi ya asilimia 51 ya bajeti ya serikali ni kulipa madeni.  Hawana namna ya kuendesha serikali ndio maana lazima walete mzigo kwenu na hatujui fedha waliyokopa wamefanyia nini kwa sababu mikataba yote ya serikali ni siri… tumebaki kukopa Jumatatu mpaka Alhamisi,” amesema.

Amesema mifumo ya kodi inaua mitaji ya wafanyabiashara wengi na kusababisha ugumu wa maisha kwa watanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

TRA yaweka rekodi makusanyo 2024, yakusanya trilioni 27.64

Spread the loveWAKATI wafanyabiashara nchini wakiweka mgomo wa siku tatu kupinga makadirio...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NSSF yawataka wastaafu watarajiwa kuhakiki taarifa zao

Spread the loveMfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) umewataka watumishi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CAG atoa kongole kwa PPAA

Spread the loveMDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles...

Habari Mchanganyiko

TRA Morogoro kuwafikisha mahakamani wafanyabiashara 27

Spread the love MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Morogoro inatarajia...

error: Content is protected !!