Sunday , 30 June 2024
Home Kitengo Biashara Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi
BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the love

Mataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti za mwaka wa fedha unaokuja huku kila taifa likielekeza nguvu kuinua nguvu ya kiuchumi, kupambana na madeni pamoja na anguko la uchumi wa mtu mmoja mmoja.

Tanzania

Kwa upande wa Tanzania, Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/2025 ambayo ni Sh trilioni 49.35 sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na mwaka wa fedha uliopita.

Akiwasilisha makadirio hayo bungeni jijini Dodoma, Dk. Nchemba ametaja vipaumbele ambavyo serikali imekusudia kuvishughulikia.

Miongoni mwa masuala ambayo yamekuwa gumzo kubwa katika siku za karibuni ni malipo ya pensheni kwa wastaafu ambapo sasa Serikali imeongeza malipo ya mkupuo kwa asilimia saba kutoka asilimia 33 ya sasa hadi asilimia 40.

Aidha, serikali ya Tanzania imelenga kuongeza wigo wa kodi na kuzingatia kanuni za usawa za utozaji kodi kwa kukusanya kodi ya zuio kwa kiwango cha asilimia tano kwenye malipo yanayofanywa kwenda kwa mtengeneza maudhui ya mtan mkazi.

Kwa mbolea za kilimo kodi itaondolewa kwa mwaka mmoja, kama itakavyokuwa kwa vifaa vya teknolojia ya michezo kama vile mfumo wa usaidizi wa waamuzi katika soka kwa kifupi VAR.

Kadhalika katika sekta ya madini kodi imefutwa kwa wafanyabishara watakaoiuzia Benki Kuu ya Tanzania madini moja kwa moja.

Hata hivyo, serikali imependeleza kuanza kwa tozo ya Sh 382 kwa kila kilo moja ya gesi inayotumika katika magari.

Kwa upande mwingine Nchemba ametetea deni la serikali ambalo linaongezeka kila kukicha na kufikia Sh 91 trilioni na kuzua mjadala katika jamii.

Waziri huyo amesema wanaoanzisha mjadala wa deni la serikali wanapaswa kutambua kuwa kukua kwa deni hilo kunatokana na sababu mbalimbali ikiwemo changamoto za kiuchumi duniani zilizosababisha sarafu ya Tanzania kushuka thamani yake dhidi ya Dola ya Marekani na kwamba fedha zinazokopwa zinatumika katika miradi muhimu ya maendeleo ya nchi.

Dk. Mwigulu Nchemba

Matarajio ya wengi yalikuwa ni kuona utitiri wa kodi unapungua na kuleta nafuu kwa watu wa kipato cha chini, jambo ambalo halijatekelezwa kikamilifu huku ikiwa ni bajeti itakayogharamia pia uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwak huu, pamoja na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo kwa ajili ya fainali za mataifa ya Afrika zitakazochezwa Tanzania, Kenya na Uganda mwaka 2027.

Kenya

Waziri wa Fedha nchini Kenya, Prof. Njuguna Ndung’u naye jana Alhamisi aliwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/2025 bungeni akiangazia maeneo ya kipaumbele kwa serikali kufikia Ajenda ya Mabadiliko ya Kiuchumi ya kutoka Chini hadi Juu (BETA).

Bajeti ya mwaka huu ilihusisha ongezeko la jumla ya matumizi ya serikali hadi Ksh.3.9 trilioni kutoka Ksh.3.6 trilioni katika mwaka wa kifedha wa 2023/24.

Waziri wa Fedha nchini Kenya, Prof. Njuguna Ndung’u.

Kati ya Ksh3.9 trilioni, Waziri huyo aliorodhesha maeneo makuu matano ya kipau mbele : Kilimo, Biashara Ndogo, Biashara Ndogo na za Kadri(MSME), Nyumba na Makazi, Huduma ya Afya na na Uboreshaji wa miundo ya Kidijitali na tasnia ya ubunifu.

Uganda

Bunge la Uganda tayari limeidhinisha bajeti ya shilingi trilioni 72.13 iliyosomwa jana.

Bajeti hiyo ya Uganda inatarajiwa kupunguza deni linaloongezeka kwa kuzingatia ukopaji wa masharti nafuu na kuzuia mikopo ya kibiashara mwaka ujao wa kifedha, waziri wake wa fedha, Matia Kasaija alisema jana Alhamisi, baada ya kushuka kwa kiwango cha mikopo mwezi uliopita.

Deni la umma la nchi hiyo ya Afrika Mashariki limekuwa likiongezeka huku serikali ya Rais Yoweri Museveni ikisitisha miradi mikubwa ya miundombinu, jambo ambalo benki kuu ya nchi hiyo imeonya.

Waziri wa fedha Uganda, Matia Kasaija

Waziri wa Fedha, Matia Kasaija alisema katika makadirio ya bajeti kuwa jumla ya deni la umma lilifikia dola bilioni 24.7 mwishoni mwa mwaka jana na lilionekana kuongezeka hadi dola bilioni 25.7 mwishoni mwa mwezi huu.

Rwanda

Wizara ya Fedha nchini Rwanda nayo jana iliweka mezani bajeti ya kiasi faranga Trilioni 5.69 ikiwa ni nyongeza ya asilimia 11.2  ikilinganishwa na ya mwaka uliopita.

Benki ya Maendeleo ya Afrika inakadiria uchumi wa kanda ya Afrika Mashariki utakua hadi kufikia asilimia 5.7 mwaka ujao hali inayoleta matumaini baada ya kipindi cha ukuaji duni wa uchumi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Biashara

Cheza sloti za Expanse kasino! mamilioni yanakusubiri 

Spread the love  Leo ni zamu yako kushinda na kuibuka Mfalme wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

error: Content is protected !!