Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mapendekezo marekebisho sheria ya habari kutinga kwa AG
Habari Mchanganyiko

Mapendekezo marekebisho sheria ya habari kutinga kwa AG

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Elieza Feleshi
Spread the love

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema mapendekezo yaliyotolewa na wadau kuhusu marekebisho ya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya 2016, yatawasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa ajili ya kutungwa muswada utakaowasilishwa bungeni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Nape ameyasema hayo leo Jumatatu, tarehe 21 Novemba 2022 katika kikao cha Serikali na wadau wa sekta ya habari cha kufanya mapitio ya mwisho kuhusu mapendekezo ya maboresho ya sheria hiyo, kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri huyo wa habari amewaeleza wadau kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ina nia ya dhati katika suala la kuboresha sheria za habari ili ziwe rafiki.

“Tupo kwa ajili ya kufanya mapitio ya mwisho ya mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari ya 2016. Niwahakikishie kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia inayo nia ya dhati katika jambo hili, nimekuja mwenyewe kuwasikiliza na imani yangu ni kuona sekta inaendelea kukua,”amesema Nape.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amesema kitendo cha Serikali kukutana na wadau kwa ajili ya kufanya mapitio ya mwisho kabla ya kutunga muswada wa sheria, kinaendelea kuonesha dhamira yake nzuri kuhusu marekebisho hayo.

‘‘Kikao kilikuwa kizuri, serikali imeendelea kuonesha dhamira yake ambayo ilikuwa nayo tangu mwanzo. Tumemaliza na serikali inaendelea na hatua zake kabla ya kupelekwa bungeni. Suala la mabadiliko ya vipengele vya sheria lina mchakato wake, cha msingi serikali imetoa fursa, na si kutoa peke yake, inaendelea kuchukua hatua,” amesema Balile.

Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile

Akielezea kwa undani kuhusu kikao hicho, Balile amesema Serikali imeonesha nia ya kukubali pendekezo la wadau la kuondoa jinai katika makosa yanayofanywa na vyombo vya habari, pamoja na pendekezo la leseni za vyombo hivyo, kutolewa kwa kipindi maalum tofauti na ilivyo sasa inatolewa kila mwaka.

Aidha, Balile amesema Serikali inakwenda kujadili pendekezo la wadau kuhusu mamlaka ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, dhidi ya vyombo vya habari, ikiwemo katika masuala ya matangazo, utoaji leseni na maudhui yake.

“Leo wamepitia yale mapendekezo moja baada ya jingine, mengi Serikali imeonesha nia ya kuyakubali lakini mpaka hapo muswada utakapowasilishwa bungeni ndio tutajua yapi yamekubaliwa,” amesema Balile.

Siku kadhaa zilizopita, Nape alisema Serikali ilishindwa kupeleka muswada marekebisho ya sheria hiyo katika Bunge la Novemba 2022, ili kutoa nafasi ya kutosha kwa wadau kutoa mapendekezo pamoja na kuyapitia kwa kina, ili ipatikane sheria bora kwa lengo kuepusha mivutano wakati wa utekelezaji wake.

Wadau walioshiriki kikao nicho ni pamoja na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Chama wa Waandishi wa Habari Tanzania (JOWUTA) na MISA- Tanzania.

Miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa na wadau wa habari kuhusu sheria hiyo, ni marekebisho dhidi ya kifungu cha 6 (e) kinachoelekeza magazeti kupatiwa leseni badala ya usajili wa moja kwa moja.

Ambapo wanapendekeza magazeti yasiendeshwe kwa kupewa leseni, badala yake yapewe usajili wa kudumu au wa muda mrefu, ili kudhibiti changamoto ya ufutwaji holela wa leseni na kuvutia wawekezaji.

Mapendekezo mengine kuhusu sheria hiyo, ni marekebishon dhidi ya kifungu chake cha 7 (2)(b)(lV), kinachoelekeza vyombo vya habari kutangaza au kuchapisha habari na masuala yenye umuhimu kwa taifa, kadiri itakavyelekezwa na Serikali , wakidai kinaingilia uhuru wa uhariri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!