Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mapendekezo mabadiliko sheria ya habari mikononi mwa AG
Habari Mchanganyiko

Mapendekezo mabadiliko sheria ya habari mikononi mwa AG

Spread the love

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema mapendekezo ya uboreshaji Sheria ya Huduma za Habari ya 2016, yamefikishwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa ajili ya kufanyiwa kazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Nape ametoa taarifa hiyo jana tarehe 27 Januari 2023, jijini Dodoma akizungumzia maendeleo ya mchakato wa marekebisho ya sheria hiyo, baada ya wadau kutoa maoni na mapendekezo yao kuhusu suala hilo.

“Kuhusu mchakato wa mapitio ya sheria za habari Namba 12 ya Mwaka 2016, nafurahi kuwajulisha kuwa baada ya majadiliano ya muda mrefu na wadau mbalimbali, hatimaye majadilioano yamekamilika na nyaraka za maeneo yote tuliyokubaliana kufanyia mabadiliko zimewasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu,”  alisema Nape.

Nape alisema kwamba maoni na mapendekezo ya wadau yamekabidhiwa katika ofisi wa AG kwa kuwa, utaratibu unaelekeza hivyo.

Alisema hatua hiyo inafanyika kabla ya Ofisi ya AG kuwasilisha Muswada wa Mapendekezo ya Sheria ya Huduma za Habari bungeni, jijini Dodoma ili kusomwa kwa mara ya kwanza, ya pili na hatimaye kupitishwa kuwa sheria.

Naye  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Taznania (TEF), Deodatus Balile alisema, mchakato huo mpaka kufikishwa bungeni una hatua zake na kwamba, inachofanya Serikali ni utaratibu wa kawaida katika kuelekea mabadiliko ya sheria hiyo.

“Mchakato bado upo kwenye mstari ule ule, mpaka sasa matumaini yetu yapo juu katika kufikia kile tunachokihitaji. Serikali bado inapitisha mapendekezo yetu katika hatua zile zile za kawaida.Sisi tungetamani kasi zaidi kama alivyoshauri Mheshimiwa Rais Samia (Sukuhu Hassan) kwamba, tulimalize,” alisema Balile.

Muungano wa wadau wa habari (CoRI) umefanya vikao viwili na serikali katika kuelekea mabadiliko ya sheria ya habari.

Wadau hao nchini wanashauri marekebisho kwenye vipengele mbalimbali vya sheria hiyo ikiwa ni pamoja na kifungu cha sita (e) kinachoeleza magazeti kupatiwa leseni kila mwaka badala ya usajili wa moja kwa moja.

Pia marekebisho dhidi ya kifungu cha saba (2) (b) (iv) kinachoelekeza vyombo vya habari kutangaza au kuchapisha habari na masuala yenye umuhimu kwa Taifa kadiri itakavyoelekezwa na serikali, wadau wakielezea kuwa kipengele hiki kinaingilia uhuru wa uhariri.

Sheria nyingine zinazolalamikiwa ni pamoja na sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na huduma za posta (EPOCA, 2010), sheria ya Makosa ya Mtandaoni (2015), sheria ya Haki ya kupata Habari (2016) na kanuni za Maudhui Mtandaoni (2018).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yapata idhini kuwa wakala wa madalali wa DSE

Spread the loveBenki ya NMB imepata idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the loveNaibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya Taifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the loveKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel...

error: Content is protected !!