Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Malisa mbaroni adaiwa kupelekwa Kilimanjaro kwa tuhuma nyingine
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Malisa mbaroni adaiwa kupelekwa Kilimanjaro kwa tuhuma nyingine

Spread the love

Mwanaharakati Godlisten Malisa,  ametiwa mbaroni  na askari wa jeshi la Polisi muda mchache baada ya kutoka kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  walipofika kwa ajili ya usikilizaji wa shauri  namba 11805 la mwaka 2024 linalomkabili. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Malisa na Meya Mstaafu wa Ubungo, Boniface Jocob (Boniyai)  wanakabiliwa na shauri la kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao.

Malisa na Boniyai walifika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo tarehe 6 Juni 2024 mbele  Hakimu Mkazi Mkuu Ushindi Swallo kwa ajili ya usikilizaji wa awali wa kesi yao .

Wakili wa serikali Happy Mwakanyamale alidai mahakamani hapo kuwa upande wa Mashtaka hautaweza kuwasilisha hoja za awali kwa kuwa mshtakiwa namba mbili hayupo mahakamani.

Mshtakiwa namba mbili kwenye shauri hilo ni Malisa ambaye alichelewa kufika mahakamani hapo.

Hakimu Swallo aliahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 4 Julai 2024 na kusema kuwa kitendo cha mshtakiwa Malisa kuchelewa kufika kwenye shauri hilo kutasababisha kufutiwa kwa dhamana yake.

Malisa alifika mbele ya hakimu Swallo kabla hajatoka kwenye chumba cha mahakama na kujisalimisha kwa Hakimu aliyemhoji sababu ya kuchelewa ambapo Malisa alimuomba radhi na kumueleza kuwa alichelewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo anauguza.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Swallo alimuonya kuwa akirudia kitendo hicho atamfutia dhamana.

Hatua hiyo imepelekea mahakama kutofuta dhamana ya Malisa lakini baada ya kutoka kwenye chumba cha mahakama askari wa jeshi la Polisi walimkamata Malisa na kumpeleka mahabusu.

Mmoja mawakili wanaowawakilisha Malisa na ‘Boniyai’ amesema kuwa mteja wake yupo mikononi mwa Jeshi la Polisi na huenda akasafirishwa kupelekwa mkoani Kilimanjaro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!